HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 13, 2020

Prof. Ndalichako aonya 'mizigo' magari mapya ya wakufunzi

   
Sehemu ya Magari 39 yaliyokabidhiwa na Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali leo Januari 13, 2020 jijini Dar es Salaam.  
Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati), akiwaongoza viongozi mbalimbali kuelekea katika eneo la uzinduzi wa magari yaliyotolewa kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali. 
Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 39 yaliyotolewa kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali. 
Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 39 yaliyotolewa kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali.   
Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati), akiingia katika moja kati ya magari 39 yaliyotolewa kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali.   
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akimkabidhi funguo ya gari Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu, Agnes Wanyankiloki, wakati wa hafla ya kukabidhi magari 39 kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Chuo cha Ualimu Ukerewe, Balbina Joseph, wakati wa hafla ya kukabidhi magari 39 kwa vyuo vya Ualimu vya serikali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akifunga mkanda wa usalama.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akiendesha moja kati ya magari 39 yaliyokabidhiwa kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali.
Kamishina wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Lyabwene Mtahabwa, akifafanua jambo katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa washirika wa maendeleo akitoa salamu.
 Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu.
Kaimu Katibu Mkuu, Moshi Kabengwe, akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.
 Waziri Ndalichako akifafanua jambo.
 Sehemu ya maafisa kutoka Wizara ya Elimu.
 Baadhi ya washirika kimaendeleo wakiwa katika hafla hiyo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi magari 39 kwa vyuo vya Ualimu vya serikali.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Moshi Kabengwe (kushoto) na Kamishina wa Elimu, Dk. Lyabwene Mtahabwa, wakionesha furaha yao baada ya waziri kutoa hotuba yake.
 Hongera kwa hotuba nzuri......ndivyo unavyoweza kusema wakati Kamishina wa Elimu, Dk. Lyabwene Mtahabwa, (kulia) akimpongeza Waziri Ndalichako.

 
Na Irene Mark

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewaonya wakuu wa vyuo 35 vya ualimu kuacha kubeba mizigo inayoongea na isiyoongea kwenye magari mapya waliyokabidhiwa leo.

Wizara ya Elimu chini ya Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo katika Sekta ya Elimu (EP4R), wanenunua magari 39 kwa thamani ya Sh. Bilioni 5.2 kwaajili ya vyuo vya ualimu, gari la Waziri na magari matatu kwa watumishi wa wizara hiyo.

Kabla ya kukabidhi magari hayo jijini Dar es Salaam leo Januari 13,2020 Waziri Ndalichako aliwataka wakaguzi na madereva wa magari hayo kutatunza ili yadumu muda mrefu na kuhudumia wengine.

"Muyatunze haya magari ni mapya kabisa msiyageuze ya kubebea mizigo ninyi mnajua kuna mizigo inayoongea na isiyoongea sitaki kusikia.

"...Mkianza kusikia gari linaleta shida usilitumie hakikisha unalitengeneza kwanza usikubali liharibike mikononi mwako," alisisitiza Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha Elimu na kwa miaka minne inefanya mambo makubwa kwenye sekta hiyo huku akisisitiza kwamba lengo ni kuhakikisha elimu ya Tanzania inakuwa bora yenye kukabiliana na ushindani kwa kutoa wahitimu bora.

Aliishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkuu wa Chuo cha Ualimu Murutunguru, Balbina Lyakurwa alisema magari hayo yataongeza chachu na kuboresha ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Pages