HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 02, 2020

HAKUNA MWENYE HATIMILIKI YA UONGOZI NDANI YA CCM: DKT. BASHIRU

Dkt. Bashiru Ally, akizungumza na viongozi wa CCM mkoani Kagera.


Na Lydia Lugakila, Kagera

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema kuwa mwaka huu ni mwaka ambao CCM itaheshimu uamuzi wa umma kutokana na chaguzi zijazo ambazo zitafanyika katika ngazi mbalimbali nchini na kuongoza siasa safi.

Alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo alikuwa akitoa salamu za mwaka mpya na mipango mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Alisema kuwa kwa sasa wanachama wa chama hicho wanaheshimu umma utakavyokuwa umeamua kama walivyoheshimu katika chaguzi zilizopita bila kupingana na uamuzi wao kwani huu ni mwaka wa siasa ambazo zitakuwa siasa safi.

Dk. Bashiru alisema kuwa kinachotakiwa ni kufanya siasa safi ambazo haziwezi kuhatarisha amani ya nchi wala machafuko yoyote ambayo yanaweza kujitokeza kwahiyo kuna umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya uuma.

Aliongeza kuwa mwaka huu ni mwaka wa kufanya siasa safi,na kujiandaa vizuri katika kuweka mazingira mazuri Sana ya kufanya siasa safi ili kusiwepo na tatizo lolote ambalo linaloweza kuleta matatizo yoyote ya siasa.

Alisema kuwa ni lazima mtu mwenye uwezo wa kutafuta uongozi kupitia itikadi yake ajiandae kikamilifu kama ambacho chama cha mapinduzi kimekuwa kikijiandaa vizuri na kuwatumikia wananchi vizuri na ndio maana kinashinda.

Aliwataka pia wanachama wa CCM kuacha siasa za ubaguzi ambazo zimekuwa zikiwagawa wanachama na kusababisha chama hicho kupoteza viti mbalimbali vya kiuongozi kutokana na migawanyiko  iliyokuwa inajitokeza hasa kwenye chaguzi za awali.

Dk. Bashiru aliongeza kuwa kama CCM inataka kufanya vizuri inatakiwa wanachama wake waache siasa za kuabudu watu na waweke nia ya siasa za kukisimamia chama na sio kutaka kuwaabudu baadhi ya watu ambao wanataka kukifanya chama ni mali yao.

"Kuna watu wana siasa za hila wao wanataka waabudiwe tu na kusema kuwa bila wao chama hakiwezi kupata mbunge au diwani na hata urais wakati kila mwanachama anaweza kuwa kiongozi kwahiyo kuna haja ya kuwakataa kwani chama kina watu wengi wenye uwezo wa kukiongoza" Alisema Dk. Bashiru.

Alisema kuwa hakuna mwenye hatimiliki ya uongozi ndani ya chama hicho kwasasa kila mwanachama anayo haki ya kugombea kwahiyo makatibu wahakikishe wanafungua milango kwa kila mtu ambaye anataka kugombea nafasi yoyote.

Katika hatua nyingine katibu huyo amewataka wanachama wa CCM wakubali pale watakapokuwa wameshindwa katika uteuzi ambao wanakuwa wameomba na wakiendelea na tabia hiyo watafuatiliwa na kuchukuliwa hatua kali za kichama.

Aliwataka wanachama kukubali kushindwa na pale wanaposhindwa na kusubiri awamu nyingine kugombee tena.
 Pia amewaomba viongozi ambao wamechaguliwa kuongoza juhudi za kuwahudumia wananchi katika maendeleo yao ya kila siku na sio vinginevyo.

No comments:

Post a Comment

Pages