Na Alodia Dominick, Misenyi
Mtoto aliyefahamika kwa majina ya Kalen Crispin (3) mkazi wa Katorelwa Tarafa ya Kiziba wilayani Misenyi ameuawa kikatili na baba yake wa kambo katika mkesha wa mwaka mpya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea Januari Mosi majira ya saa 6:40 usiku wakati mama wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Domina Endrew ambaye aliolewa na Leonardi Kishenya wakati mtoto huyo akiwa mdogo.
Kamanda Malimi ameeleza katika mkesha wa mwaka mpya mke na mume walitoka kwenda kunywa pombe waliporudi nyumbani ulianza ugonvi kati ya wanandoa hao baada ya ugomvi huo kudumu kwa muda ndipo mama wa marehemu alikimbilia kwa majirani na kulala huko na kumwacha marehemu amelala.
Aliporudi nyumban majira ya saa moja asubuhi alikuta mtoto ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na katika mkono wa kushoto alikuwa na majeraha mbalimbali.
Mama wa marehemu alitoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji na kisha polisi ndipo ulifanyika upelelezi wa tukio hilo na Januari 2, 2020 polisi walimtia mbaroni Leonardi Kishenya baba wakambo wa mtoto huyo na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Kamanda Malimi ameutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kupoteza maisha ya viumbe ambavyo havina hatia.

No comments:
Post a Comment