HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2020

KIWANDA CHA KAGERA SUGAR KUONGEZA UZALISHAJI

Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba (katikati), akipata maelezo alipotembelea Kiwanda cha Kagera Sugar.


 
Na Alodia Dominick, Misenyi
 
Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, amevitaka viwanda vinavyozalisha sukari kuongeza kasi ya uzalishaji kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watanzania ili kuacha kutumia sukari ya nje ya nchi.

Akizungumza katika kiwanda cha Sukari cha Kagera kilichopo wilaya ya Misenyi Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, alisema kuwa richa ya tani 450,000 zinazohitajika kila mwaka kwa ajili ya Watanzania bado kiasi hicho hakizalishwi hapa nchini badala yake zinazalishwa tani 350,000 kwa mwaka kiwango ambacho hakikidhi mahitaji ya watanzania na hivyo wakati mwingine kuna watu huomba vibari kwa ajiri ya kutoa sukari nje ya nchi ingawa wamekuwa siyo waaminifu na hivyo baadhi yao huomba vibari vya tani ndogo na kuingiza sukari nyingi nchini.

Mgumba amesema ili kudhibiti hali hiyo ya kuingiza sukari kutoka nje ya nchi ni lazima viwanda vya hapa nchini vizalishe sukari kwa wingi kwa ajili ya kukidhi matakwa ya watumiaji.

"Kama mnataka tudhibiti uingizaji wa sukari kutoka nje ni lazima viwanda vyetu vya sukari ambavyo viko hapa nchini kwetu tuzalishe sukari kwa wingi ili itosheleze matumizi ya wananchi wetu tayari tumeishaweka mikakati ya kuzalisha sukari ya kutosha kwenye viwanda vyetu kilichobaki ni wenyeviwanda kutekeleza mikakati hiyo".
Alisema Mgumba

Na kuongeza kuwa wamejiwekea mikakati na viwanda vinavyozalisha sukari kuwa tatizo la kupungua kwa sukari liwe limeisha kwa muda mfupi.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Vincent Mtaki, amesema kwamba, kwa mwaka 2020 wanatarajia kuzalisha tani elfu 95 ambapo kwa mwaka jana walizalisha tani elfu 80 na katika mpango wa miaka mitano 2020 hadi 2024 kiwanda kitazalisha tani laki moja na elfu themanini (180,000).

Mtaki amesema takwimu ya uzalishaji wa sukari itaongezeka kutokana na mashamba mapya ambayo yameanzishwa katika pori la kitengule hekali elfu 28 ambazo kila heka inazalisha tani 60 hadi 80 za sukari.

Kwa upande wake Salma Msonga anayehusika na maswala ya  kilimo kiwandani (Ignomist) amesema kuna aina ya miwa iliyokuwa inazalishwa kiwandani hapo na ilikuwa inatoa mavuno kidogo tani hamsini kwa hekta lakini kwa sasa wanayo miwa ya aina mbalimbali ambayo huzalisha tani 60 kwa 80 kwa hekta moja.

No comments:

Post a Comment

Pages