HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2020

BILIONI 25 KUTUMIKA UJENZI WA DARAJA-KARAGWE


Na Alodia Dominick, Misenyi

Zaidi ya shilingi 25 bilioni zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa daraja linalounganisha wakulima wa miwa wanaotoka wilaya ya Karagwe kuja Misenyi ambapo kuna kiwanda cha Kagera Sugar.

Fedha hizo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano baada ya Rais John Magufuri kutembelea kiwanda cha Kagera Sugar na kuona umbali uliokuwa ukitumika kutokea eneo la Karagwe kuja kiwandani kuwa mrefu kutokana na mto Kagera ndipo aliamua lijengwe daraja hilo.

Msimamizi  wa eneo hilo upande wa kilimo kutoka kiwanda cha Kagera Sugar, Abubakari Hamisi, ameeleza kuwa daraja hilo lilijengwa ili kusaidia kuunganisha mashamba ya miwa ya Kiwanda ambayo yako Kitengule wilaya ya Karagwe.

Amesema Daraja likikamilika watatumia  kilomita 10 kutoka Kitengure kuja Kagera Sugar wakati awali walikuwa wanatumia kilomita 60 kutoka kiwandani kwenda upande wa pili wa mto Kitengure.

"Tunamshuru rais Magufuri kuona umuhimu wa kujenga daraja la kuunganisha wilaya mbili Karagwe na Misenyi kwani usafirishaji wa miwa kutoka kitengule utatumia gharama nafuu". alisema Hamisi

Amesema hatua za ujenzi zinaendelea na wanatarajia daraja likikamilika wakulima upande wa Karagwe watanufaika kuleta miwa na wataongeza wigo wa ajira.

Kwa upande wake Naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba amesema kuwa serikali ilikubaliana kuwekeza asilimia 10 kwenye sera ya kilimo.

Mgumba ameitaka kamati ya ulinzi na usalama wilayani Misenyi kujenga kituo cha polisi kwenye eneo linapojengwa daraja kutokana na tatizo la magendo ya kahawa ili uwepo udhibiti.

Naye Meneja wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Vincent Mtaki, amesema kutokana na wakulima kuwauzia miwa katika kiwanda hicho wamekuwa wakikutana na changamoto ya kuwapatia mbolea wakulima ili wazalishe miwa ya kutosha na badala yake wakulima hao wamekuwa wakiuza hiyo mbolea.

Ameeleza kama kiwanda kwa kushirikiana na halmashauri ya Misenyi kupitia wamekuwa maafisa kilimo wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi ya mbolea kwenye mashamba ya miwa inavyoongeza uzalishaji.

No comments:

Post a Comment

Pages