Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT
- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati alipoitwa Kituo cha Polisi Wete, Pemba.
Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT
- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati alipoitwa Kituo cha Polisi Wete, Pemba.
Baadhi ya wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad wakimsubiri wakati akihojiwa na Polisi.
Na Talib Ussi, Zanzibar
Jeshi la Polis Mkoa wa
Kaskazini Pemba limewaachia kwa dhamana Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT
- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Habari,
Mawasiliano ya Umma, Salim Biman, kwa madai ya kufanya mkusanyiko kinyume na
sheria katika eneo la Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara ya kumaliza kumhoji Maalim Seif, Kamanda wa Polisi
Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis, alisema waliwaita viongozi hao kwa kufanya mkutano wa hadhara Desemba 9, 2019 huku wakijua mikutano yote imezuiwa.
“Mkutno huo ulikuwa wa
ndani, lakini waliufanya wa wazi jambo ambalo halikuwa na uhalali wa kisheria”,
alieleza Khamis.
Alisema kuwa
viongozi hao wote wameaachiwa kwa dhamana bila ya kutaja siku ya kurudi kituoni
na kueleza kuwa na jalada wameshalipeleka kwa DPP kwa hatua zaidi.
Kwa upande wake Maalim Seif alisema anashangaa kuaambiwa kuwa wamefanya mkutano wa hadhara kwa
kile alichoeleza kuwa mkutano wao ulikuwa wa ndani na nje kufunga maturubali
ili kuwadhibiti watu wao.
“Sisi tumepangua hoja
zote kwa sababu hazina mashiko, watu wetu sisi wote walikuwa ndani na ambao
walikuwa nje hatukuwa na dhamana nao”, alisema maalim Seif.
“Tumewaambia kuwa
Polisi ule sio mkutano wa nje, kwa sababu mkutano wa nje lazima utangazie
watu kila kona lakini sisi hatujatangazia mtu” aliendelea.
Alieleza kuwa
alipokwenda Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dk. Bashiru Ali, kisiwani baadhi ya
barabara zilifungwa lakini jeshi hilo halikueleza chochote na badala yake
wanafanyakazi ya CCM kudhibiti mtu ambaye hawamuwezi.
“Kwa hiyo nakuombeni
wananchi msiwe na wasiwasi sisi tuko salama na tutaendelea kufanya shuhuli
zetu kisiasa kwani zipo kisheria”, alisema
Maalim Seif.
Baada ya kutoka kituoni
hapo Maalim Seif alipokelewa na wanachama na wananchi waliokuwa nje ya kituo.
Mamia ya wafuasi wa
chama hicho walijitokeza nje ya kituo wakipiga mayowe ya kumtaka kiongozi wao,
na Jeshi la Polisi kuwaamuru waondoke bila kufanikiwa.
"Tunalishauri Jeshi la
Polisi liache kutumika kisiasa mwenendo wake ni dhahiri linatumiwa na CCM.
“Sisi kazi yetu ni
kulinda kituo chetu hatuwezi kuwaingilia watu walio nje ya kituo, ambao
wana shauku na viongozi wao”, aliendelea.
Kwa upande mwingine Katibu wa Mipango na Wanachama wa chama hicho, Omar Ali Shehe na Katibu wa Mkoa
wa Kusini Pemba na waliitwa na Jeshi hilo mkoni humo kujibu hoja kama hizo.
No comments:
Post a Comment