HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 14, 2020

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAIPIGA JEKI HOSPITALI YA RUFAA IRINGA

Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation Doris Mollel akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa huku mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation Doris Mollel baada ya kukabidhi vifaa vya tiba.
Hivi ndio vifaa ambavyo vimetolewa na taasisi ya Doris Mollel mkoani Iringa.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA

KATIKA kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake taasisi ya Doris Mollel (DMF) inayojihusisha na maswala ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wametoa msaada vifaa mbalimbali kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Taasisi hiyo imetoa msaada wa mashine tatu za kupumulia kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda,magauni 30 ya Kangaroo ambayo wamama wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum dhidi ya watoto wao ikiwemo kupata joto la Mama, mipira 1000 ya kulishia watoto njiti, sabuni za unga,mipira 100 ya kusafirishia hewa kutoka katika mashine za kupumulia na pampas za watoto vyote vikiwa na thamani ya sh. Milioni 11.5.

Akizungumza mkoani Iringa Mkurugenzi wa DMF, Doris Mollel, alisema  kwa kutambua umuhimu kwa sababu wanawakumbuka  watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na kutoa msaada huo ni kutaka  kuokoa uhai wa watoto hao .

“Kutambua thamani ya watoto njiti tumeona katika kuokoa uhai na kuweza kufikia malengo tumeona ..mashine za kuwasaidia kufikia malengo yao kama walivyo watoto wengine…taasisi itaendelea kutoa mchango kwa jamii,” alisema Doris.

Mollel  alisema kuwa msaada huo una lengo kubwa la kuwasaidia watoto hasa watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.

“Tumeamua kufanya hivi kwa lengo la kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabbla ya wakati wasipoteze maisha hivyo taaisis nyingne na watu wengine waweze kuwakumbuka watoto hawa na kuweza kuwasaidia kuweza kuokoa maisha yao na kuwafanya waishi kama watoto wengine katika maisha na kutimiza ndoto zao kama ambavyo mimi nilizaliwa njiti na sasa najitoa kwa moyo mmoja kuweza kuwasaidia” alisema

Aliongeza kuwa kiwango cha vifo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya kukomaa nchini  huchangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa vifaa vya kutosha kusaidia mifumo yao ya upumuaji mara tu wanapozaliwa hivyo kama mmoja ya watoto hao ambaye nilibahatika kupata msaada na huduma ya kutosha nilipozaliwa natambua jinsi gani matunzo haya ya awali yalivyo muhimu kwenye kuokoa maisha ya watoto hawa na kuwasaidia.

Alisema kwamba moyo huo wa kutoa msaada unatoka ndani ya moyo kwa kuwa alipozaliwa alikuwa njiti na bila kupata msaada ndoto za maisha zisizingekuwepo hivyo taasisi hiyo imejitoa katika kusaidia mashine hizo kuweza kuwakoa watoto wengi zaidi nchini ambapo wamezifikia hospitali 33 nchini hadi sasa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na ilihudhuriwa na Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa, Dk. Alfred Laison Mwakalebela ambapo walishukuru kwa msaada huo kwa hospitali ya Iringa na kutoa wito kuendelea kuwa na moyo wa kusaidia zaidi katika hospitali mbalimbali nchini.

Kasesela alisema kuwa kitendo ambacho taasisi ya Doris Mollel cha kujitolea kufanya kazi za kuwasaidia watoto waozaliwa kabla ya wakati ni Baraka kubwa kutoka kwa MUNGUna msaada huo utasaidia kukusanya na kuonyesha matatizo ya wahitaji ili kuongeza uelewa na msukumo wa misaada kutoka kwa sekta binafsi na wanajamii kwa ujumla kuliko kusubiri serikali kufanya hivyo.

“Tunatambua mashine hizi ni bei kubwa na Serikali pekee yake haiwezi kufanya hivyo kwa kusaidiana na wadau kama hivi ni faraja sana na tunapongeza juhudi hizi za taasisi ya DMF kwa kujitokeza kusaidia mashine kwa watoto njiti na kutoa wito kuendelea kusaidia zaidi bila kukata tamaa kuahidi serikali kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo” ameeleza Mkuu wa Mkoa huyo.

Kwa upande wake mganga mfawadhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa , Dk Alfred Laison Mwakalebela alisema kuwa kuanzia Januari hadi Disemba 2019 hospitali hiyo ililaza watoto njiti 544 kati ya hao 292 walikuwa watoto ambao walizaliwa na uzito pungufu ambao wanakuwa na matatizo kama watoto njiti na watoto 252 waliozaliwa njiti.

Alisema kuwa watoto hao wanapozaliwa wanakabiliana na kupumua kwa shida kutokana na mapafu kutokomaa na kushindwa kunyonya vilevile wanapata sana maambukizi mbalimbali ndio maana wanapiga marufuku watu kuingia katika wodi za watoto hao na wanakosa sukari mwilini kutokana na kutokula sawasawa.

Alisema kuwa 2019 watoto waliozaliwa njiti walikuwa 252 na kati ya hao watoto 15 walifariki na kupunguza idadi ya vifo vya watoto hao ukilinganisha na miaka ya nyuma na kutokana msaada wa awali wa mashine hizo zilizotolewa na taasisi hiyo na kuwa jengo la wadi la pekee la watoto hao na utaalam watoa huduma sawa na asilimia mbili.

Dk Mwakalebela alisema kuwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa watoto 20 hadi 25 wanazaliwa kwa mwezi hivyo bila kuwa na vifaa vya kuwasaidia wanaweza kupoteza maisha kwahiyo msaada uliotolewa na taasisi ya DMF ni mkubwa ambao utasaidia kupunguza na kuondokana na vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

No comments:

Post a Comment

Pages