HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 01, 2020

MBUNGE PROF. MUHONGO AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA KUPIGA KASIA MUSOMA VIJIJINI

 Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo akimkabidhi zawadi  ya Kombe la ushindi katika mashindano ya kupiga kasia yaliyofanyika katika Ziwa Victoria Kijiji cha Bukima,Musoma Vjijini mwishoni mwa mwaka 2019.
 Mmoja wa washindi wa mashindano hayo (kulia), akipongezwa kabla ya kukabidhiwa kombe la ushindi wa mashindano ya hayo ya kupiga kasia.
 Mmoja wa washindi akikabidhiwa zawadi ya Kombe huku akiashangiliwa na wenzake.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano hayo.
 Wananchi wakishuhudia mashindano hayo.


Na Mwandishi Maalumu
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amekabidhi zawadi za vikombe na fedha taslimu kwa washindi wa mashindano ya Kupiga Kasia (The Annual Boat Race) yaliyofanyika mwishoni mwaka jana katika Kijiji cha Butima, Ziwa Victoria jimboni humo.


Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameamua kwa vitendo kufufua  Utamaduni na Michezo jimboni mwao iliyokuwa inafifia  na kuanza kutoweka., ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya  CCM 2020, jimboni humo. 

Kila Mwaka, Mbunge huyo anatayarisha na kufadhili mashindano ya Kwaya (nyimbo) na Ngoma za Asili.

Vilevile, Mbunge huyo ni mmoja wa wafadhili wa timu ya mpira ya Mkoa wa Mara, Biashara United inayoshiriki Ligi Kuu ya Taifa. Ameombwa na kukubali kuna mmoja wa Wafadhili wa WASAGA FC ya Kata ya Nyamrandirira itakayoshiriki Ligi ya Daraja III. Mbunge huyo alishagawa Vifaa vya Michezo Vijijini na Mashuleni.


Akitoa salamu za mwaka mpya mbunge huyo alisema kuwa "Mwaka Mpya (2020) uwe ni Mwaka wa Maarifa mapya, Ubunifu mkubwa, Ushirikiano mkubwa, na Utekelezaji wenye umakini na ufanisi mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages