Na Mauwa Mohammed, Zanziibar
Mkurugenzi wa chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA), Dkt. Mzuri Issa, amevitaka vyama vya siasa kuwandaa wanawake ili waweze kugombea nafasi za tofauti za uongozi.
Akizungumza na wadau wa vyama vya siasa wakati wa kuwasilisha ripoti ya utafiti iliyofanywa kwa vyama vya siasa ili kubaini changamoto zinazowakwaza wanawake katika kugombea nafasi za uongozi.
Mkurugenzi huyo alisema katika vyama vya siasa kuna mapungufu mengi ambayo yanamkwaza mwanamke na kupelekea kushindwa kugombea nafasi za uongozi.
Akiwasilisha ripoti hiyo Edi Issa kutoka Youyth Foroum alisema wanawake wanakabiliwa na changamoto ya tamaduni, silka ,hali ya uchumi kuwa duni pamoja na wanawake wenyewe kutokujitambua na kupelekea kushindwa kugombea nafasi za uongozi.
Alisema mfumo wa vyama vingi unaonekana ni uadui wakati Tanzania imo katika mfumo wa vyama vingi na pia wanawake wasomi hawako tayari kuingia kwenye siasa kutokana na kukosa mashirikiano kutoka kwa jamii.
Aidha alisema pia wanawake wanakumbwa na changamoto ya ukosefu wa rasilimali fedha na woga wa kutolewa kashfa zinazoweza kumvunja moyo wakati anaposimama mbele kwa nia ya kujieleza.
Wakichangia washiriki wa mkutano huo walisema wanawake wanaotaka kugombea nafasi wapewe elimu ili wapate kujielewa na pia wanaume na wao wajengewe uwezo ili na wao waweze kujua umuhimu wa viongozi wanawake.
Akiwasilisha mazimio ya mkutano huo Afisa Sera na utafiti wa TAMWA Haura Shamte amesema Tanzania imeridhia mikataba mingi ya kimataifa ikiwemo azimio la SADEC linalosema ifikapoi 2030 tayari kila nchi iwe imefikia asilimia 50% ya wagombea wanawake katika nafasi za uongozi.
“Kwa kuanzia mwaka 2020 kuwepo mikakati angalau iwe tayari imeshafikia angalau asilimia 40 iwe wanawake wamegombea kwenye nafasi za uongozi wa mabunge na wawakishi ili kufikia malengo ya mkataba huo”alisema Bi Haura.
Pia serikali imetakiwa kuweka mazingira rafiki na salama kwa wagombea inapofika wakati wa uchaguzi ili wagombea wanawake waondoshe hofu na woga katika kugombea nafasi hizo.
“tunaviomba Vyama vitoe vipeperushi ili kumpa kipaumbele mwanamke anapogambea achaguliwe” alisema Haura.
Bi haura akitoa maoni kwa niaba ya Tamwa alishauri kufanywe mapitio ya Muongozo wa kamati ya madili ili kulinda mwanamke na suala la ukatili na udhalilishaji akiwa mgombea au kampeni meneja na ziwepo kanuni ili kuona mwanamke analindwa katika siasa na wakati wa uchaguzi.
“Imeonekana vyama vya siasa havitoi nafasi muafaka kwa watu waliopembezoni wakiwemo wanawake na watu wenye ulemavu hivyo Vyama vya siasa vijipange vitoe nafasi kwa watu wenye ulemavu wa aina zote” aliendelea Haura.
Tamwa kwa kushirikiana na asasi za kiraiya wameandaa mkakati wa kutafuta changamoto zinowakwaza wanawake ili kuziondoa na badala yake wapate kugombea nafasi za uongozi bila woga.
No comments:
Post a Comment