Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za Motisun Group, Subhash Patel, akigonganisha chupa na Balozi wa kinywaji cha Twist, Rajab Abdul ‘Harmonize’, wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Motsun Group inayosambaza Sayona Drinks imetangaza kinywaji kipya cha Twist Avatar.
Kampuni ya Sayona imedhamiria kuwapa machaguo mengi zaidi wateja wake ili kukidhi hitaji la |adha mbalimbali zinazopendwa na wateja.
Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa bidhaa hiyo, Pawan Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa Sayona Drinks Limited alisema, ”Twist ni kiburudisho chenye ladha nzuri, kinachokupa thamani ya pesa yako ikiwa na |adha saba za kipekee ikiwemo ya Pasheni, Chungwa, Limao, Embe, Nanasi, Tangawizi na ladha ya Cola,”
Patel alibainisha kuwa Kampuni itatangaza ujio wa ladha nyingine za kipekee katika siku za baadaye na kuongeza kuwa, Sayona, imedhamiria kukidhi hitaji la wateja wake ndiyo maana wameendelea kuwa wabunifu na kila mwaka wamekuwa wakitambulisha bidhaa mpya sokoni.
“Tunaamini kupitia Twist, tunayo bidhaa hora ambayo ina utofauti na bidhaa nyingine zilizopo sokoni, kuwapa wateja wetu kiburudisho chenye ladha nzuri na ya kipekee,"alisema.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Drinks Ltd Group, Nitin Menon, alizungumzia juu ya utoaji wao huduma kwa wateja na gharama za bidhaa hiyo mpya.
Menon alisema, hatua ya kuizindua Twist ni matokeo ya kazi kubwa inayofanyika ya kuimarisha ukuaji wa kampuni kupitia mkakati kabambe ambao unaenda sambamba na badiliko la ladha kwa watumiaji na tabia katika ununuzi.
"Bidhaa yetu mpya ya Twist inakuja kwa ujazo wa milimita 300 na 400 katika chupa ya plastiki. Bidhaa itauzwa kwa bei ya rejareja ya shiiingi 500 na itapatikana nchi nzima," aliongeza.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuutangazia umma kuwa. wameingia makubaliano na staa wa bongo fleva Rajabu Abdul Kahali ‘Harmonize’ kuwa balozi wa heshima wa bidhaa za Sayona ambaye pia alishiriki katika uzinduzi huo.
“Tunajisika fahari kuwa na Harmonize kama balozi wa heshima wa bidhaa yetu. Ni miongoni mwa Vijana wapambanaji, mwenye msaada kwa watanzania wengi, anayefanya kazi kwa bidii, lakini pia amekuwa chachu ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbali zaidi. Hili ni Jambo ambalo linaunga mkono malengo na maono yetu ya kuwa kinara katika biashara ya vinywaji baridi barani Afrika," alisema Menon.
“Tuna imani kwamba ushirikiano huu utawezesha vinywaji vya Sayona kuwa miongoni mwa bidhaa zenye nguvu zaidi Tanzania. Harmonize atatusaidia kuwafikia walengwa wetu nchini Tanzania na sisi kufanya naye kazi kama balozi, ni miongoni mwa hatua muhimu ya yeye kushiriki katika miradi yetu mingi inayokuja."
Kwa upande wa Harmonize, alisema “ni jambo la faraja kufanya kazi na Sayona Drinks Limited na huu ni mwanzo wa ushirikiano mzuri zaidi baina yake na kampuni.
Akizungumzia juu ya uzinduzi wa bidhaa hiyo. Harmonize alisema, ”Twist ni kinywaji kizuri chenye ladha za kipekee mmekuwa nikikitumia mara kwa mara na nimekuwa sehemu ya ubunifu huu mpya wa bidhaa hii, nina hakika kuwa Watanzania watafurahia bidhaa hiyo na matumizi yake yatafika nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment