HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 14, 2020

MNH-MLOGANZILA KUJENGA KITUO CHA UPANDIKIZAJI WA VIUNGO VYA BINADAMU NCHINI

 Mtaalam kutoka kitengo cha Radiolojia MNH-Mloganzila, Dkt. Ahmed Sauko akielezea namna mashine ya MRI inavyofanya kazi.
 Muuguzi Rose Chasuka akielezea namna mashine ya kupima mapafu inavyofanya kazi wakati wa ziara hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi (katikati) akitoa taarifa wakati wa ziara hiyo.



Na Andrew Chale

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila inatarajia  kujenga kituo cha Umahiri cha upandikizaji Viungo (Centre of Excellence  for Organ Transplant) kitakachosaidia kupunguza makali ya gharama kwa Watanzania walizokuwa wakizifuata nje ya Nchi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Dkt.Julieth Magandi amesema hayo leo  wakati wa taarifa yake kwa Maafisa habari waandamizi wa Taasisi za Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto waliopo kwenye ziara ya kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Tano inayojulikana kama 'TUNABORESHA SEKTA YA AFYA'.

Ambapo amebainisha kuwa, tayari bajeti ya fedha Serikali ya Awamu ya Tano imetenga na kinatarajiwa kujengwa katika eneo jirani na Hospitali hiyo ya Mloganzila.

"Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali imetenga fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 8 kwa ajili ya uanzishwaji wa kituo cha Umahiri cha Upandikizaji viungo.
Kitaalamu tunaita 'Centre Excellence for Organ Transplant' na vitu vingi vitapandikizwa hapa" alisena Dkt. Magandi.

Amevitaja viungo ambavyo vitapandikizwa katika kituo hicho kitakapokamilika ambapo kitasaidia Watanzania wengi kufuata huduma nje ya Nchi  ni pamoja na :

"Upandikizaji wa Ujauzito (In Vitro fertilization-IVF) na pia huduma ya kupandikiza Uloto (Bone marrow).


Pia kutakuwa na upandikizaji wa  Ini (Liver Transplant), Macho (Corneal transplant), Figo (Kideney transplant).
Na kituo cha wataalam kujifunzia (Skills lab)" alisema Dkt. Magandi.

Aidha, akielezea mipango iliyopo ni pamoja na ujio wa huduma ya upandikizaji Uloto (Bone marrow transplant) huduma ambayo itaanza kutolewa kwa mara ya kwanza hapa nchini.

"Katika maboresho na kuongeza huduma kwa Watanzania.  Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Muhimbili-Upanga tunatarajia kuanzisha huduma ya upandikizaji Uloto. Huduma hii itaanza kutolewa Februari mwaka huu na hii itakuwa ya kwanza hapa nchini kwani haiakuwepo".  Alisema Dkt. Magandi.

Aidha, katika kuburesha huduma za Wagonjwa mahututi (ICU), wapo mbioni kupokea wataalam  Sita kutoka Nchi ya Cuba ambao wamebobea kwenye huduma hizo huku pia wakitarajia kuwa msaada mkubwa kwa wataalam wazawa wa ndani ambao watapata ujuzi kutoka kwao.

Hadi sasa Hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa mbalimbali na kuhudumiwa na ikiwemo kupata tiba za kibingwa.

"Kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa nje (OPD) kutoka 17,116 katika robo mwaka ya Julai hadi Septemba 2018 na kufikia wagonjwa 24,945 katila robo mwaka ya Oktoba-Desemba 2019 sawa na ongezeko la asilimia 46.

 huku wagonjwa wa ndani wakiongezeka kutoka 1,459 katika robo mwaka ya Julai  hadi Sepremba 2018 na kufikia wagonjwa 2,419 katika robo mwaka ya Oktoba hadi Desemba 2019 sawa na ongezeko la asilimia 66". Alisema Dkt. Magandi.

Hospitali hiyo ya Muhimbili-Mloganzila ilifunguliwa rasmi Novemba 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa chini ya uendeshaji wa Chuo kikuu cha Afya na tiba shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) iliyochini ya wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia na

baadae Oktoba 3,2018 ilikuja kubadilishwa usimamizi na uendeshaji kuhamishiwa wizara ya Afya na kuwa chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili hivyo kuitwa 'Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.

No comments:

Post a Comment

Pages