HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2020

SIMBA vs YANGA NCHI ITASIMAMA DAKIKA 90

 Nahodha wa Simba, John Bocco, akizungumzia maandalizi ya pambano lao na Yanga. (Picha na Simba SC).
 Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck, akizungumzia pambano lao na Yanga.


Na John Marwa

WASWAHILI wanasema asiye na Mwana aeleke Jiwe, Ndivyo itakavyokuwa kesho kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Simba SC dhidi ya Yanga SC watatoana jasho kusaka pointi tatu muhimu za Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).

Wakati Watanzania hasa mashabiki wa Simba na Yanga wakisubiri kushuhudia dakika 90 za kibabe,  makocha na manahodha wa timu hizo wamezidi kuwaita mashabiki wao kwenda kuwasapoti.

Kocha wa Simba, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck, akizungumza na Waaandishi wa Habari leo amesema anatambua mchezo utakuwa mgumu lakini kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mchezo huo.

“Tuko tayari kwa ajili ya mechi na kila mmoja anaisubiri kwa hamu, tunatambua huu mchezo ni mkubwa na mgumu hivyo maandalizi yote yamekamilika, kikubwa mashabiki wa simba wajitokeze kushuhudia burudani.”amesema Sven.

Kwa upande wa kocha wa Yanga Charles Boniface Mkwasa, amesema kikosi chake kiko timamu kwa ajili ya kupambana huku akiwataka mashabiki wa klabu ya Yanga kutokuwa wanyonge kuelekea mchezo huo.

“Sis tumejiandaa na tuko tayari kwa ajili ya mchezo huo hata wakitaka leo sisi tunautaka kwa sababu tunajiamini na tuko tayari kwa ajili ya mapambano, kikubwa wasije na matokeo yao mifukoni mpira ni dakika 90”

Kwa upende wa Manahodha wa timu zote mbili John Bocco Simba na Juma Abdul Yanga, wamewataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia burudani itakayo tolewa na pande zote mbili.

“Kama wachezaji tumejianda vena kikubwa tutaenda kutekeleza maagizo ambayo tumepewa na benchi la ufundi kwa ajili ya hii mechi, mashabiki wetu wajitokeze kwa ajili ya kupata burudani, tunawaahidi hatutawaangusha” John Bocco.
“Mpira ni dakika 90, hivyo kama wachezaji tuko tayari hata sasa kwa ajili ya mchezo, kikubwa niwaombe mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi, wasiogope maneno ya mtu yeyote yule sisi wachezaji tuko tayari tutawapa wanachostahili.” Abdul.

No comments:

Post a Comment

Pages