HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2020

WANANCHI BUKOBA WADAI KUOBWA RUSHWA ILI KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA


Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Godfrey Mheluka, akizungumza na wananchi wilayani humo.




Na Lydia Lugakila, Kagera

Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Karagwe mkoani Kagera imewataka wananchi wanaofuatilia suala la vitambulisho vya Taifa (NIDA) kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika kama wanaombwa Rushwa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Godfrey Mheluka, ambapo amesema kuna baadhi ya madai kuwa kuna baadhi ya  wananchi hao wameombwa  pindi wanapokuwa wanafuatilia namba hizo hasa kwenye ofisi za kuhojiwa za uhamiaji.

Akizungumza na wananchi waliokuwa wakifuatilia namba zao mkuu huyo wa wilaya amesema katika siku za hivi Karibuni amepokea taarifa ambazo zinaendelea kufanyiwa uchunguzi zinazodai kuwa  baadhi ya wananchi wanaombwa rushwa na baadhi ya maofisa ya uhamiaji huku akiwaonya watumishi hao kuwa wakibainika hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao.

"Ninazo taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba watu wakienda kule uhamiaji wanaombwa fedha kiasi cha shilingi elfu 50, wewe utakayetoa Pesa na yule  atakayepokea mtakamatwa na kamera zitafanyakazi"alisema Mheluka.

Amesema mpaka sasa uchunguzi wa kubaini tuhuma hizo unaendelea huku akiwataka wananchi kutokulipa fedha zozote wakati wakiendelea na mchakato huo kwani zoezi hilo ni bure.

Aidha kwa upande wake Afisa wa NIDA wilayani Karagwe, Rabson Sifuni, amesema zoezi la kutoa vitambulisho kwa wananchi zinaendelea vizuri kwani kwa siku moja zaidi ya wananchi 120 hupatiwa huduma.

No comments:

Post a Comment

Pages