Mshambuliaji raia wa Brazil, Wilker Da Silva, akiwa mazoezini wakati akiichezea Simba.
Msemaji wa Simba, Haji Manara, akzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo.
Na John Marwa
KLABU ya Simba rasmi imeachana na Mshambuliaji raia wa Brazil Wilker Da Silva kwa kutoridhishwa na kiwango chake.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, katika mkutano na vyombo vya Habari leo jijini Dar es Salaam.
Senzo amesema Wilker ni mchezaji mzuri lakini ameshindwa kuendana na Soka la Tanzania jambo ambalo limepelekea ashindwe kuinyesha makali yake.
"Napenda kuwataarifu kuwa ni rasmi sasa tumeachana na Wilker da Silva kwani ameshindwa kuonyesha kile timu inachohitaji kutoka kwake.
"Wilker ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji lakini Soka la Tanzania limekuwa changamoto kwake, siku mbili zilizopita ameondoka kuelekea Norway kuna timu amepata huko, tu amtakia kila la heri "
Senzo ameongeza kuwa Simba iko kwenye mchakato wa kusaka nyota wawili au watatu ambao watakuja kuongeza nguvu kikosini.
Amesema licha ya muda kuwa mchache lakini uongozi unajitahidi kufuata taratibu watu sahihi kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.

No comments:
Post a Comment