Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
nchini (TARI), Dk. Geofrey Mkamilo, ambaye pia mratibu wa kuamasisha upandaji wa michikichi
nchini akikabidhi sehemu ya mbegu za
mchikichi zenye uwezo wa kutoa mafuta ya mawese kwa wingi na zinakua kwa muda
mfupi ,mbegu hizo zimekabidhiwa elfu
hamsini 50,000 kwa SSP Dominic Kazimili ambaye ndiye Mkuu wa Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma ikiwa njia ya kuteketeza agizo
la waziri mkuu katika kupunguza uagizaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
nchini (TARI), Dk. Geofrey Mkamilo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo
pichani juu ya mikakati ya kuzalisha mbegu milioni tano ifikapo june 2020
ambapo mpaka sasa wameshazalisha mbegu milioni 1.2.
Mkurugenzi
wa kituo cha utafiti wa michikichi TARI Kihinga Dk. Philison Kagimbo, anaelezea
kitaalamu jinsi ya uzalishaji wa miche ya michikichi ya Tenela yenye uwezo
mkubwa katika utoaji wa mafuta ya kula ambapo moja ya mchakato wake ni pamoja
uwekwa katika pipa na kufukiwa chini na kuwekewa mkaa ili kupata nyuzi joto 40 kusaidia ukuaji wa
miche kwa haraka.
Sehemu ya
mbegu 50,000 zilizokabidhiwa na Taasisi
ya utafiti wa kilimo TARI kwa gereza la Kwitanga mkoani Kigoma ,ambapo mbali TARI
kukabidhi mbegu katika gereza hilo pia ameshakabidhi kwa halmashauri sita za
mkoa wa kigoma na jeshi la kujenga taifa JKT Bulombola.
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Wakulima wa michikichi mkoani kigoma wamefuraishwa
na hatua ya serikali kugawa bule mbegu
za muda mfupi na zenye tija katika ukamuaji wa mafuta ya mawese ya zao la michikichi
aina ya Tenela badala ya mbegu za zamani ambazo utumia zaidi ya miaka kumi
mpaka kuanza uzalishaji.
Wakulima hao wamesema mara baada ya taasisi ya utafiti wa kilimo
nchini TARI kugawa zaidi ya mbegu 50,000 katika jeshi la Magereza Kwitanga kwa
lengo la kutekeleza agizo la serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika
kuboresha uzalishaji wa zao la mchikichi ili kupunguza tatizo la kuagiza mafuta
ya kula kutoka nje ya nchi
Akikabidhi mbegu hizo kwa maafisa wa jeshi la
magereza Kwitanga mkurugenzi mkuu wa TARI Dkr Geofrey Mkamilo amesema wameshaotesha
mbegu za kisasa la zao la mchikichiki zaidi ya milioni 1.2 zenye uwezo wa kutoa
mafuta kwa wingi na kuota kwa muda mfupi ambazo zitagaiwa kwa wakulima na taasisi za
serikali bule na zimesaidia kuokoa zaidi
ya bilioni 5.4 ambazo zingetumika kununua mbegu hizo.
Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa kilimo
nchini TARI dkr Geofrey Mkamilo ambae ndio mratibu wa kuamasisha upandaji wa
michikichi nchini amesema Tanzania inahitaji mafuta ya kula tani laki 570 huku
yanayozalishwa nchini ni tani laki 205
na kusabaisha kutumia shilingi bilioni 443 kwaajili ya kuagiza tani laki 365 ili kukidhi hali ya mafuta ya kula
hapa nchini.
Ambapo uwoteshaji na Ugawaji wa miche ya michikichi katika mkoa wa Kigoma kutokana
na agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa unaendelea kwa kasi huku wanatarajia
mpaka ifikapo June 2020 zaidi ya miche milioni 5 itakuwa imeoteshwa kwaajili ya
kupewa wakulima.
No comments:
Post a Comment