HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 01, 2020

WATOTO SABA WAZALIWA MKESHA WA MWAKA MPYA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA KAGERA

Na Lydia Lugakila, Kagera

Jumla ya watoto saba wamezaliwa katika mkesha wa mwaka Mpya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera huku hali za watoto hao na mama zao zikiripotiwa kuendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari muunguzi wa zamu wa wodi ya wanawake katika hospitali hiyo, Dickson Vedasto, amesema kati ya watoto hao sita ni wa kike na mmoja ni wa kiume.

Vedasto amesema kati ya watoto hao waliozaliwa mtoto mmoja amezaliwa kwa njia ya upasuaji na hali ya mama yake inaendelea vizuri.

Aidha muuguzi huyo amesema hali za watoto na mama zao zinaendelea vizuri na wakati wowote wataweza kuruhusiwa na kurejea majumbani kwako.

Hata hivyo amewahimiza akina mama wajawazito kutojifungulia majumbani kwani madhara yake ni mkubwa badala yake wafike katika hospitali au vituo vya afya ili kupata huduma yenye uhakika.

No comments:

Post a Comment

Pages