Na Irene Mark
MAMLAKA
ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza tukio la kupatwa kwa mwezi
kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 2:07 usiku wa Januari 10 hadi saa 6:17
usiku wa kuamkia Januari 11,2020.
Taarifa ya
kupatwa kwa mwezi ilitolewa Dar es Salaam leo Januari 9, 2020 na Meneja
wa Utabiri wa Kituo Kikuu cha Utabiri, Samuel Mbuya na kusema ni tukio
nadra kutokea kwa muda mrefu hivyo kuwataka watanzania kushudia sayansi
hiyo ya anga.
"Tukio hili litaonekana kwa
sehemu kubwa kwenye nchi ambazo muda huo utakuwa usiku hasa Ulaya, Asia,
Australia na Afrika...hili tukio huonekana wakati dunia, mwezi na jua
vikikutana kwenye mstari mmoja mnyoofu.
"Mwezi
huanza kupungua mng'ao wake na kuwa giza kabisa kwenye uso wa dunia kwa
muda kisha hurudi kwenye hali yake ya kawaida, hakuna athari kubwa
zinazoweza kutokea ingawa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji
baharini kwa sababu ya mvutano kati ya maji na mwezi kwenye bahari,"
alisema Mbuya.
Alitumia muda huo kuwashauri
wanafunzi wa masomo ya sayansi kufuatilia tukio hilo la kidunia na
kujifunza zaidi kuhusu sayansi ya anga.
No comments:
Post a Comment