Mwenyekiti wa EASD, Abdallah Khamis (katikati), akiwa katika picha ya kumbukumbu.
Na Mwandishi Wetu, Kibiti
MAKUNDI
ya kina mama vijana na walemavu nchini, wametakiwa kutumia vizuri
mikopo inayotolewa na halmashauri mbali mbali kwa ajili ya kuinua maisha
yao kiuchumi pamoja na uchumi wan chi.
Wameelezwa
kuwa mikopo hiyo kwa makundi hayo ni nafuukwa kuwa haina masharti
magumu kama ile inayotolewa na taasisi za kifedha, hali inayowafanya
watu wengi kushindwa kupata.
Hayo
yalielezwa juzi wilayani Kibiti na CPA.Janeth Kikoty,katika semina ya
siku moja iliyoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Education
Agender for Sustainable Development(EASD),kwa kushirikiana na chama cha
wahasibu Tanzania(TAA),ambapo wajasiriamali wa vikundi 16 walishiriki
CPA
Kikoty,alisema dhamira ya serikali ni kuona kila mwananchi anafanikiwa
hivyo umakini, uaminifu na na kujituma kwa kila anayepata mikopo hiyo
kutaiwezesha nchi kufikia uchumi wa viwanda
“Uaminifu
ni nguzo kwenu mnaopata mikopo lakini ni vema pia mkaniwekea mazoea ya
kukagua mahesabu yenu kila baada ya kipindi Fulani ili mjue kama
mnasogea mbele ama kurudi nyuma”alisema CPA Kikoty.
Katika
semina hiyo mkurugenzi wa mipango na elimu wa chama cha wahasibu
Tanzania CPA. Ezekiel Stephen, alisema chama hicho kipo tayari
kuwasaidia watanzania mbali mbali katika suala zima la uelewa wa
utunzaji wa mahesabu ya fedha kitaalam na kwamba huduma hizo wanazifanya
pasipo kuhitaji gharama kutoka katika vikundi vya wajasiriamali
“Sisi
TAA tupo tayari kuwasaidieni nyie wajasiriamali kuwapa mafunzo ya namna
bora ya kuhifadhi kumbu kumbu zenu za kimahesabu na hili hatulifanyi
kwa gharama yeyote pale mtakapokuwa mmejikusanya na kuhitaji elimu
hii”alisema CPA.Ezekiel.
Aliongeza
kuwa jambo la muhimu kwa makundi yanayohitaji elimu hiyo ni kufuata
utaratibu mzuri wa namna ya kuwafikia katika maeneo wanayokusudia
kupatiwa elimu hiyo
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa EASD, Abdallah Khamis, alieleza kuwa jukumu
kubwa la taasisi yake ni kuhakikisha wanawaunganisha wadau mbali mbali
na kuwafikishia elimu mtambuka kulingana na mahitaji husika ya wakati
huo
“Tulipata
taarifa kuwa mnapewa mikopo na Halmashauri sisi kama taasisi yenye
jukumu la kutoa elimu tukawatafuta wenzetu wa TAA na kuwaomba watusaidie
wataalam wao kwa ajili ya kuja kuwapa mafunzo haya mnayoyafanya
leo”alisema Khamis.
Aliongeza
kuwa EASD ni taasisi iliyojipambanua kutoa elimu mtambuka kwa
kushirikiana na wataalamu mbali mbali na kwamba huo ni mwanzo wa dhamira
yao hiyo.
Awali
afisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Kibiti Anthony Nyange alisema
wameshawapatia vikundi 17 mikopo yenye thamani ya sh. Million 40,
kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake vijana na walemavu, fedha
zilizotoka katika bajeti ya mwaka 2019-20.
Fedha tulizowakopesha leo ni sehemu ya fedha za mfuko wa maendeleo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”alisema Nyange.
No comments:
Post a Comment