HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 18, 2020

WANANCHI KAGERA WAOMBA KUONGEZEWA MUDA USAJILI WA LAINI ZA SIMU

    Diwani wa Kata Kanyigo, Mh. Walter Nyahoza.


Na Lydia Lugakilas, Kagera

Zikiwa zimesalia siku mbili za kila raia wa Tanzania kuhakikisha anasajili laini za simu ya mkononi ili kupata Kitambulisho cha Taifa (NIDA) wananchi wa Kata ya Kanyigo wilayani Misenyi Mkoani Kagera wameziona siku hizo kama mazingaombwe na kuziomba mamlaka zinazohusika  kuongeza siku.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Kanyigo  iliyopo wilayani Misenyi Mkoani Kagera, Walter Mwesigwa Nyahoza, ambaye amekuwa akipokea malalamiko kila kukicha kutoka katika kata hiyo ili apeleke kilio hicho kwa Rais wa Dkt. John Magufuli ili kuongezewa siku kutokana na changamoto kadhaa.
 
"Tangu kuazishwa kwa zoezi hilo tangu mwaka 2018 zoezi hilo limekubwa na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa watendaji wa NIDA na Uhamiaji waliojiandikisha tangu kuanza kwa zoezi hilo ni wananchi 4500 na waliopata namba ya  NIDA wakiwa ni 720," Walisema wananchi hao.

Diwani Walter Nyahoza amesema kuwa kutokana na zoezi hilo kugubikwa na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa watendaji wananchi hao wamemuomba Rais Magufuli kuongeza siku ili kila mwananchi atimize wajibu huo.

Diwani huyo amesema licha ya kutumia muda mwingi kuhamasisha wananchi hao kujiandikisha bado hali ni tete.

"Amesema wananchi hao wametumia muda mwingi na gharama nyingi, kufuatilia vitambulisho hivyo bila mafanikio na kuiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa undani kwa kuongeza muda," alisema.

Kata ya Kanyigo iliyopo wilayani Misenyi ipo matatani kupokea watu wasio raia wa Tanzania kwani wako mpakani na jinsi zoezi lilivyo na uharaka.

Akitaja adha kubwa wanayoipata wananchi amedai kuwa wameanza kujiandikisha upya muda ambao wangepata namba na vitambulisho, kwenda kila siku katika vituo hivyo kupanga foleni asbh   hadi jioni, ubovu wa barabara ya Kamagosho Mgana unaopelekea Magari  kutopita kuelekea katika zoezi hilo.

Aidha amesema waliofanikiwa katika zoezi hilo la kupata namba bila vitambulisho wengi ni viongozi na wafanyakazi wa serikali na kumuomba Rais Magufuli ili zoezi hilo liwe endelevu hadi nchi nzima itakapokamilisha usajili huo.

Kwa mujibu wa viongozi wa NIDA kituo kingine  kimeongezwa katika kata ya Bwanjai walipo watu wengi ambacho kinakwenda tarafa ya kiziba inayojumuisha kata kumi.

Diwani wa kata hiyo amelazika kutumia shilingi 600,000 ili kuwawezesha watendaji wa zoezi hilo kwa ajili ya chakula na maradhi.

Hata hivyo Diwani huyo ametoa pongezi kwa serikali  katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 800 katika kata hiyo ukiwemo mradi wa kuhudumia kaya masikini, barabara, maji na kumalizia maboma katika kipindi cha mwaka 2015- 2019.

No comments:

Post a Comment

Pages