HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2020

WANANCHI TUNZENI MIRADI YA MAJI-FAHODE

 Mwenyekiti wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Faraja for Hope and Development (FAHODE), Antiduis Augustine, akizungumza na wananchi.
 Diwani wa Kata ya Ibwera, Ahmed Kiobya, akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
 Andochius Rutahiwa Kamuhabwa ambaye ni mwezeshaji wa shirika hilo akizungumza na wananchi.
Wananchi wakisikiliza viongozi.
 
 
Na Lydia Lugakila, Kagera

Watumiaji wa maji Kata za Ibwera, Katerero na Katoro Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kuondoa vikwazo na malalamiko katika miradi ya maji vinavyosababisha maendeleo  kurudi nyuma badala yake waitunze na kuijali miradi pamoja na kuthamini nguvu zinazotumika katika uwekezaji wa miradi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Faraja for Hope and Development (FAHODE) Antidius Augustine katika mkutano wa hadhara uliowaunganisha wananchi pamoja na viongozi mbali mbali wa kata hizo wakati wa upokeaji wa taarifa ya mrejesho wa ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika sekta ya maji.

Katika taarifa hiyo mwenyekiti huyo amesema licha ya juhudi za viongozi hao katika kuboresha na kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo bado wananchi hao ambao ni walengwa wa miradi hiyo wanaendekeza vikwazo na malalamiko yasiyokuwa na tija huku wakiwa hawaitikii mikutano pale inapohitishwa hali inayosababisha ujumbe unaokuwa umekusudiwa kutofika kwa walengwa.

Mwenyekiti huyo amesema wananchi hao wanatakiwa kuacha malalamiko badala yake washirikiane vyema na viongozi ili kuhakikisha ya miradi haikwami huku akitaja baadhi yao kutoudhuria mikutano kwa wakati na wakati mwingine kikosa kabisa.

Augustine ameongeza kuwa nguvu nyingi hutimika kuwekeza katika miradi ya wananchi ikiwemo fedha nyingi kutumika hivyo wanahitajika kuilinda, kuitunza kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo akitoa taarifa fupi ya FAHODE amesema asasi hiyo imeisaidia jamii pakubwa kwani tayari miradi mbali mbali imewafikia walengwa.

Kwa upande wake mwezeshaji wa shirika hilo Andochius Rutahiwa Kamuhabwa amewasihi wananchi hao kuwajibika ipasavyo    katika kuitunza miradi ya maendeleo na kuwa hawapaswi kuwasubiri viongozi waliopo madarakani.

Hata hivyo Diwani wa kata ya Ibwera Ahmed Kiobya amesema kila mwananchi ahakikishe anakuwa mlinzi wa miradi ya maendeleo kwa kutoruhusu mtu au watu watakaovuruga, kuiba na kuharibu miradi.

No comments:

Post a Comment

Pages