Na Mwandishi Wetu, Mlali Dodoma
WAKAZI wa Kata ya
Mlali waliohojiwa kwa nyakati tofauti wameiomba Serikali Kuu impe haki ya
kusikilizwa aliyekuwa Mganga, Henry Gwerino, aliyepasua wajawazito 1,600 bila
vifo kufuatia kuondolewa kwenye wa Kituo cha Afya Mlali Utumishi wa Umma kwa
madai ya kuwasilisha vyeti vya kughushi!.
Wengi waliotoa hoja hiyo
ni akina mama ambao waliwahi kuwa na matatizo ya akina mama na wengine ujauzito
ambao walipasuliwa na kupata mafanikio ya kurejeshewa afya zao, hivyo
waliposikia kuondolewa katika utumishi wa umma kwa mganga huyo walitoa neno.
Katika barua yake ya
malalamiko ya 05/07/20119 kwa Katibu Mkuu OR kwenye Tume ya Utumishi wa Umma
akiomba arejeshwe kazini Gwerino alisema, “Kipindi nipo kazini nimeweza kufanya
upasuaji wa dharula kwa akina mama wajawazito zaidi ya 1,600 bila kusababisha
kifo chochote”.alisema Gwerino alijenga hoja ili arejeshwe kazini.
Kupitia barua Kumb.
Na. HW/KOG/CF.S.20/1VOL.VII/153 YA 11/07/2018 Gwerino alikiri aliandikiwa barua
na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambayo ilimuondoa
kwenye utuminishi wa umma kutokana na kuwakilisha nakala ya cheti cha kughushi
cha Kidato cha Nne.
Hata hivyo Wakazi hao
walidai, kama zoezi la kuhakiki vyeti liliwahusu wafanyakazi walioajiriwa
kuanzia mwaka 2004 kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya Kanuni za Utumishi wa umma za
2003 ikisomwa pamoja na Kanuni D.12 ya Kanuni za kudumu za utumishi wa umma za
2009 katika kuhitimisha Ajira za watumishi, mbona huyu aliajiriwa 1982 na zoezi
hilo halimhusu? Waliohoji!.
Pamoja na hoja za
wakazi hao, ikumbukwe Gwerino alikiri Katibu Mkuu OR Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala bora katika barua Kumb. Na. CFC.26/205/01/06 ya 13 Aprili 2018
kwa watumishi walioghushi vyeti au kuandika taarifa za uongo katika kumbukumbu
zao, aliagiza utaratibu huo ufuatwe katika kusitisha ajira za watumishi.
Aidha Gwerino alidai, mbali
ya Tume ya utumishi wa umma kukiri kupokea malalamiko yake kwa barua Kumb.Na CCB.81/125/01/11
ya 05/08/2019 ilimrejeshea Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
suala hili kwa mujibu wa maelekezo rasmi ya serikai yaliyotolewa na Katibu Mkuu,
Utumishi kama ilivyorejewa ikimtaka kuwasilisha vielelezo vinavyoonesha namna alivyohitimisha
shauri hili, jambo ambalo Gwerino anasema hajapata maelekezo yoyote.
“Tume inasubiri,
maelekezo ya ufafanuzi kutoka kwa mwajiri wako. Unatakiwa kusubiri wakati suala
linashughulikiwa” alisema hayo ndiyo maagizo aliyopewa lakini alidai hadi leo hajapata
maelezo yoyote na wananchi wanasema wanahitaji huduma yake iwasaidie lakini
yeye anawataka wawe na Subira.
No comments:
Post a Comment