HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2020

BENKI YA CRDB YADHAMINI KONGAMANO LA UWEKEZAJI MKOA WA SONGWE



KONGAMANO la Uwekezaji, lililoandalia na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Mstaafu, Nicodemus Mwangela, limeafunguliwa leo Februari 16, 2020 mjini Vwawa, Mbozi, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kongamano hilo linalodhaminiwa na taasisi kadhaa, ikiwemo Benki ya CRDB, linafanyika kwa siku tatu likitanguliwa na Semina Elekezi, iliyoendeshwa na mkuu huyo wa mkoa, ambako linafikia kilele Februari 17, 2020 katika viwanja vya CCM Vwawa, Mbozi.

Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa, Waziri Kairuki, aliwataka wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia furtsa za kiuchumi zilizopo mkoani Songwe, ambao ni lango kuu linalounganisha nchi za Jumuiya ya SADC.

Kairuki alizitaja fursa mbalimbali ambazo zinapatikana Mkoa wa Songwe kwa kuwahusisha wadau wa uwekezaji kuwa ni sekta ya madini, kilimo na utalii kwa kuwataka kuchangamkia fursa zilizomo mkoani humo. 

Waziri Kairuki aliipongeza CRDB kwa kuwa mdau mkubwa katika kuleta chachu ya maendeleo nchini Tanzania, kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawawezesha wadau na sekta mbalimbali nchini kwa kutoa mikopo nafuu ya uwekezaji. 

Aidha aliwataka wawekezaji Songwe na nchini kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo na Benki ya CRDB, ambayo ni moja ya wadhamini katika kongamano hilo.

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki (katikati), akikabidhi cheti cha kutambua mchango wa Benki ya CRDB katika kufanikisha Kongamano la Uwekezaji Mkoa wa Songwe. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi wa Benki ya CRDB, Nuru Kateti na kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Denis Mwoleka. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki, akisalimiana na Meneja Mwandamizi wa Taasisi wa Benki ya CRDB, Nuru Kateti, alipotembelea Banda la CRDB. Kushoto ni Meneja wa CRDB Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Denis Mwoleka.
 
Meneja Mwandamizi wa Taasisi wa Benki ya CRDB, Nuru Kateti, akizungumza katika Kongamano la Uwekezaji mkoani Songwe.
 Wateja mbalimbali wakipata huduma kutoka kwa maofisa wa Benki ya CRDB walipotembelea Banda la benki hiyo katika viwanja vya CCM mkoani Songwe katika Kongamano la Uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Mstaafu, Nicodemus Mwangela, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la CRDB kukagua na kupata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Denis Mwoleka (wa tatu kulia). Wengine ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi wa Benki ya CRDB, Nuru Kaketi na kulia ni Meneja Mahusiano Idara ya Mikopo, Uwezeshaji wa Biashara, Mathias Mushi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Mstaafu, Nicodemus Mwangela, akikagua banda la CRDB.
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Mstaafu, Nicodemus Mwangela, akipata maelezo kwa Meneja Mwandamizi Wateja wa Serikali wa Benki ya CRDB, Nuru Kaketi (kulia).
 Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo, akifurahia jambo huku akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya CRDB. Kulia ni Meneja wa CRDB Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Denis Mwoleka.

No comments:

Post a Comment

Pages