Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki, akimkabidhi cheti
maalumu Afisa Mkuu kwa Wateja Binafsi Biashara Ndogo na za Kati wa NMB -
Filbert Mponzi wakati wa Kongamano la Uwekezaji lililofanyika katika
viwanja vya Vwawa Mkoani Songwe.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji - Angela Kairuki amewata wawekezaji wa ndani na
nje ya nchi kutumia fursa ya Mkoa wa Songwe kuwa lango la nchi za SADC kwa kwenda kuwekeza katika sekta mbalimbali
zilizopo Mkoani humo hasa katika sekta ya Kilimo ili kuinua uchumi wa Mkoa huo na nchi kwa
ujumla.
Angela alisema hayo jana wakati alipokuwa akizindua
kongamano la uwekezaji Mkoa wa Songwe, lililofanyika katika kiwanja cha
Vwawa Wilayani Mbozi. Aliongeza kuwa, Mkoa huo una fursa nyingi ambazo zimeanishwa za
biashara na uwekezaji zinazotokana na kuwekwa kimkakati na viongozi wa Mkoa kwa
kuwa kiungo kati ya Tanzania na nchi zaidi ya 16 za SADC.
Aidha alisema kuwa, katika suala la uwekezaji Mkoa uhakikishe
unatenga meaneo ya uwekezaji katika kila Halmshauri kwa kuweka miundo mbinu
mbalimbali ili kumrahisishia mwekezaji pindi anapoenda kuwekeza katika Halmashauri.
Awali akimkaribisha
Mgeni rasmi katika kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe - Brigedia General
Nicodumus Mwangela alisema, Mkoa wa Songwe umeaandaa kongamano lenye lengo la kutangaza fursa na
vivutio vya uwekezaji vilivyopo katika Halmashauri zote za Mkoa huo ili kuvutia
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Aidha,
mmoja wa wadhamini wa kongamano hilo Benki ya NMB - Filbert Mponzi
ambaye ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara Ndogo na za Kati
alisema kuwa Benki yake imetoa jumla ya shilingi bilioni 22 katika Mkoa
wa
Songwe kwenye sekta ya kilimo hasa katika mazao ya kahawa ,mahindi na
mengine
yanayolimwa Mkoani humo.
Alisema kuwa, kwa mwaka huu benki hiyo imeanza kufungua
akaunti kwa ajili ya wakulima ambapo ni wito wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa wakulima wote lazima walipwe
kwenye akaunti zao na kuwa akaunti hizo
zitafunguliwa bure ili wakulima wote
waingie katika mfumo ambao uko rasmi.
Mponzi
alisema kuwa benki ya NMB imeanza kutoa mikopo kwa
wajasiliamali yenye riba nafuu lakini hata yenye dhama ambazo siyo
rasmi, ikiwa na
lengo la kuwawezesha wajasiliamali wadogo wote waweze kunafaika na
mikopo ya
benki, hivyo hata kufuatia mikopo hiyo wanaimani watatokea wawekezaji wa
kati
hata wadogo Mkoa Songwe watakaoenda kupata mkopo NMB. Katika uwekezaji
wake Benki hiyo imefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 400 kwa
wajasilimali wadogo na wakati.
Mbali na kusaidia wajasiliamali lakini pia benki hiyo imekuwa ikisaidia katika miradi
mbalimbali hapa nchini na kuwasaidia wakandali mbalimbali ambapo mpaka sasa wametoa dhamana kwa
wakandalia wa ndani zaidi ya mia 400 kupitia uhusiano walionao na TARURA.
Afisa huyo alimuhakikishia Waziri huyo kuwa watashirikiana
na Mkoa wa Songwe katika kuhakikisha wawekezaji wanasaidiwa katika benki yao
pindi watakapoenda kwa ajili ya kutaka huduma mbalimbali za kifedha ilikwa na
lengo la kuhakikisha Mkoa wa Songwe unakuwa kiuchumi kupitia wawekezaji wao.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment