HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2020

UFUGAJI WA MBWA, KILIMO WAMPATIA UTAJIRI KIJANA EVANCE

Kijana Evance Kamenge akisimulia  alivyopambana na ajira.

Na Lydia Lugakila, Kagera

Kijana
Evance Kamenge, aliyepambana na ukosefu wa ajira kwa muda mrefu ametoa neno kwa Serikali baada ya kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana 1,000.


Evance Kamenge aliyeanzisha ufugaji wa mbwa na kilimo cha miti amebainisha hayo mbele ya Naibu Waziri Ofisi Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira Sera na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, katika kongamano la Umoja wa Vijana CCM mkoani Kagera lililofanyika katika ukumbi wa Linas uliopo Manispaa ya Bukoba na  kuwakusanya vijana toka wilaya nane za mkoa huo.

 amesimulia  alivyopambana na suala la ajira pamoja na kipato hadi kufikia hatua ya kujipatia ajira na kisha kuajiri vijana 1,000, Evance ambaye kwa sasa ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za Kilimo amesema ameamini ajira sio ofisini.

Hatua hiyo imekuja kufuatia vijana wengi kulilia ajira kila kukicha na kubaki kuilaumu serikali.

Kijana huyo amesema mwanzoni alianzisha ufugaji wa Samaki na kuku akiwa anasambaza bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam ambapo baadae akajikita katika ufugaji wa Ng'ombe ambapo pia aliaweza kusambaza  majiwa jijini Dar es salaam na kupata mafanikio makubwa na kuamua kuanzisha biashara ya ufugaji wa mbwa wa aina mbali mbali kutoka Afrika kusini na sasa ni msambazaji wa wanyama hao ndani na nje ya Nchi kama Zimbabwe, Zambia.

Amesema biashara hiyo ya mbwa imependwa sana na watu kutokana na kwa ajili ya ulinzi wao binafsi na makampuni mbalimbali.

Amesema hadi sasa taswira ya maisha yake imebadilika sana ambapo akiwa mkoani Kagera katika harakati za kilimo cha miti maharage na mahindi ametoa ajira 1000 kwa vijana.

Katika kuboresha ufugaji wa mbwa amesema tayari kwa mkoa wa Kagera ameanzisha ofisi yake maeneo ya Custom ambapo ameanza kujenga mabanda ili kushawishi vijana kuingia katika ufugaji wa mbwa.

"Mbwa ni uchumi mbwa ni fursa nimepata gari, nimejenga nipo katika harakati za kuendesha shule moja hapa Kagera na nitatoa mafunzo kwa vijana juu ya kuendesha miradi mbali mbali "lisema Kamenge.

Aidha amemuomba Naibu Waziri kuhakikisha wizara hiyo inatambua mashindano kama ya kwake yaliyoleta mafanikio kwa vijana 1000 kupata ajira.

Hakika kilimo ni utajiri sasa kilimo na ufugaji wa mbwa vimefanya  maisha ya Kijana Evance Kamenge kuwa tajiri.

Kwa upande wake Naibu Waziri huyo amepongeza juhudi za kijana huyo na kuahidi kuzungumza naye kwani tayari amekuwa mdau mkubwa kutokana na upambanaji huo.

Waziri Mavunde amesema bado ipo changamoto kubwa kuwakusanya vijana watano mpaka kumi wenye mlengo mmoja na kuwa baadhi ya maeneo vikundi vikundi vingi vinashindwa kuendelea ambapo vijana uchukua mkopo kama wa milioni 5 kwenda kugawa na kununua viatu badala ya kuwekeza katika shughuli za kimaendeleo.

Hata hivyo amesema serikali itaendelea kuwasaidia vijana wote wakiwemo wenye ulemavu kwa kufanya marejeo ya kanuni za utoaji mikopo ili vijana wanufaike na fursa.

No comments:

Post a Comment

Pages