Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi
wa CCM Taifa, Humphrey Polepole katika mkutano wa Kuadhimisha miaka 43 ya CCM
wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, ameeleza kuwa Wamefuatilia mijadala na
mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya Upinzani kuhusu kufanya maridhiano, Polepole
anaeleza maridhiano ni hatua na vyama vya upinzani nchini vimeshindwa tangu
mwanzo na hata sasa kuzingatia hatua za msingi na za awali kabla ya kufikia
hatua ya maridhiano
na hivyo kukosa uhalali wa kutaka
maridhiano, kwani maridhiano huanza kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo
ya msingi, pili kujenga muafaka na tatu kuwa na maridhiano yenyewe.
Akifafanua kuhusu dhana na
nadharia ya maridhiano, Polepole amesema, kwanza kuwepo na uelewa wa
pamoja juu nini watanzania wanataka, kazi kubwa ya maendeleo ambayo imekwisha
kufanyika nchini na kubadilisha kabisa hali na ustawi wa watu, pili ni kuwa
muafaka wa kitaifa kwa maana ya kukubaliana katika kazi nzuri ambayo imefanyika
na katika yale ambayo hakuna muafaka ndio tunakwenda katika maridhiano.
Awali akihutubia mkutano huo wa
maadhimisho ya miaka 43 ya CCM, Polepole ameeleza ni kwa namna gani Chama
cha Mapinduzi kimejipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, huku akiangazia
mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 43 ya CCM na kwa umahsusi mafanikio ya
serikali ya awamu tano chini ya John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.
Kauli mbiu ya Miaka 43 ya CCM ni
Tuliahidi, Tumetekeleza na Tunaahidi Tena kuchapa kazi kwa juhudi, Ubunifu na Maarifa
Zaidi
No comments:
Post a Comment