Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kesho February 11 kuanzia Saa Mbili Asubuhi anatarajiwa
Kuzindua Rasmi Wilaya Mpya ya Kigamboni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa Wingi
katika Uzinduzi huo wa Kihistoria.
RC
Makonda amesema hafla ya Uzinduzi huo inatarajiwa kuanza Saa Moja
Asubuhi kwenye Viwanja vya Mkuu wa Wilaya ambapo Rais Magufuli atazindua
Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya, Jengo la Halmashauri na Majengo ya
Hospital ya Wilaya ya Kigamboni.
Uzinduzi
huo unakuja wakati muafaka ambao Tayari Serikali imefanya juhudi kubwa
za Maendeleo katika Wilaya hiyo kupitia Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi
wa Barabara za Lami, Ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati,
Huduma za maji, Elimu pamoja na huduma zote muhimu.
No comments:
Post a Comment