HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 05, 2020

Serikali kuanzisha shule za mahitaji maalum kila mkoa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Ave Maria Semakafu (wa pili kushoto), akimuangalia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Dodoma, Enock Mabawa, ambaye ni mlemavu wa macho, jinsi anavyotumia tarakilishi ‘kompyuta’ wakati wa kufunga Mafunzo ya Matumizi ya Tehama na vifaa saidizi kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu wa sekondari wenye mahitaji maalum, yaliyofanyika Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Ave Maria Semakafu (wa pili kushoto), akifafanua jambo wakati wa kufunga Mafunzo ya Matumizi ya Tehama na vifaa saidizi kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu wa sekondari wenye mahitaji maalum, yaliyofanyika Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), jijini Dar es Salaam.
 Darasa la Kompyuta.
 Mwakilishi wa walimu waliopata mafunzo akitoa hotuba yake.
 Mkuu wa Kitengo cha Tekonojia Saidizi Chuo Kikuu Huria (OUT), Mhadhiri Mwandamizi Dk. Cosmas Mnyanyi, akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya walimu waliopata ya Mafunzo ya Matumizi ya Tehama wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Ave Maria Semakafu. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Ave Maria Semakafu, akitoa hotuba yake wakati wa kufunga Mafunzo ya Matumizi ya Tehama na vifaa saidizi kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu wa sekondari wenye mahitaji maalum, yaliyofanyika Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), jijini Dar es Salaam.
 


Na Irene Mark

 
SERIKALI imejipanga kuanzisha shule za watu wenye mahitaji maalum wakiwemo viziwi kila mkoa hapa nchini.

 
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Avemaria Semakafu alipokuwa akifunga mafunzo ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na vifaa saidizi kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu wa sekondari wenye mahitaji maalum.

 
 Mafunzo hayo waliyopatiwa wakufunzi na walimu wa sekondari wasioona, viziwi na wenye ualbino yalilenga kuwajengea uwezo katika matumizi ya Tehama na teknolojia saidizi ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha ufundishaji katika vyuo vya ualimu na shule za sekondari hapa nchini.

 
Semakafu alisema azma ya Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kila mkoa na baadae wilaya zinakuwa na shule hizo maalum ili wenye mahitaji wapate mafunzo mbalimbali ya kuendeleza ujuzi wao na mwisho wa siku waweza kujiajiri au kuajiriwa.

 
“Watu wenye mahitaji maalum wamegawanyika, wapo wengine ni rahisi kuwachanganya darasani ila wapo wengine ni vugumu wakiwemo  viziwi niwe mkweli tu... sio vizuri kuwachanganya darasani kwa sababu  wenyewe masiko yao ni macho na macho yao ni macho na ukienda kwenye takwimu zao vipindi vyao vinatakiwa visizidi dakika 15.

 
"Natoa wito kwa jamii msiwabague watu wenye mahitaji maalum, ulemavu wao si kikwazo katika ufanyaji wa kazi mbalimbali," alisema Semakafu.


Akizungumzia mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Tekonojia Saidizi Chuo Kikuu Huria (OUT), Mhadhiri Mwandamizi Dk. Cosmas Mnyanyi alisema wamejipanga kutoa elimu ya teknolojia saidizi ambayo yanaondoa changamoto za kazi kwa wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment

Pages