HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 24, 2020

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA SH. MILIONI 30 KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA CORONA (COVID-19)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 30 Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha Osati, ikiwa ni msaada wa Benki ya CRDB kusaidia kampeni ya kuelimisha juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona. Hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika katika tawi la Benki ya CRDB Azikiwe, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akinawa mikono kwa kutumia vitakasa mikono wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 30 kwa Chama cha Madaktari Tanzania, ikiwa ni msaada wa benki hiyo kusaidia kampeni ya uelimisha juu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha Osati, akinawa mikono ikiwa ni tahadhari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Sh. Milioni 30 kwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT),  kwa ajili ya kusaidia kampeni ya uelimisha juu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiagana na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha Osati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,  akizungumza na wateja wa Tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,  akizungumza na wateja wa Tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,  akizungumza na wateja wa Tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam.
 Wateja wa Benki ya CRDB wakinawa mikono kabla ya kuingia katika tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.



Na Mwandishi Wetu

Benki ya CRDB imetoa msaada wa shilingi milioni 30 kwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corana. Akizungumza katika hafla fupi na waandishi wa habari iliyofanyika katika tawi la Azikiwe, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema msaada huo unakwenda kusaidia kampeni maalum inayoendeshwa na chama hicho katika kuelimisha Watanzania juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona (COVID-19) ijulikanayo “TUNAWEZA KUJIKINGA”.

Nsekela alisema katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na ugonjwa wa Corona hakunabudi kwa taasisi na mashirika yote kuungana na Serikali na wataalamu wa afya katika kutoa elimu kwa Watanzania itakayosaidia kupunguza maambukizi na kuondokana kabisa na ugonjwa huo wa Corona.

“Benki yetu ya CRDB tayari imeshachukua hatua mbalimbali zinazosaidia kuwakinga wafanyakazi na wateja wetu, ikiwamo kuweka dawa za kusafisha mikono (hand sanitizer) katika ofisi zetu, matawi pamoja na ATM,” alisema Nsekela huku akishukuru Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari kwa kuwa nao bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Elisha Osati aliishukuru Benki ya CRDB kwa mchango huo wa shilingi milioni 30 huku akisema kuwa hela hiyo itaelekezwa katika kuelekezwa katika utoaji elimu kwa watumishi wa sekta ya afya husasan katika huduma za afya za msingi kuanzia Zahanati na Vito vya Afya itakayowasaidia kutambua wagonjwa na hatua za kuchukua pindi wanapopata mgonjwa. Dkt. Osati alisema zoezi hilo linaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Madaktari kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanafanzi (TAMSA), ambapo zoezi hilo tayari limeshaanza katika mkoa wa Dar es Salaam.

“Wajibu wetu nikuhakikisha madaktari, wauguzi na watumishi wote wa sekta ya afya wanakuwa na elimu ya kutosha ya kupambana na ugonjwa huu. Tukiweza kuwafikia hawa itasaidia elimu hii kusambaa kwa Wananchi wengi na hivyo kuepukana kabisa na ugonjwa huu wa Corona,” alisema Dkt. Osati huku akiwataka na wadau wengine kuungana Benki ya CRDB.

Hafla hiyo pia iliambatana na zoezi la uhamasishaji wa kunawa mikono kwa wananchi ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa kushirikiana na Raisi wa Chama cha Madaktari, Dkt. Elisha Osati na Katibu wa cha hicho, Dkt. Lilian Mnabwiru waliochesha namna bora ya kunawa mikono, huku wakiwahamasisha Watanzania kunawa mikono mara kwa mara ikiwa ni njia ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.

“Katika mapambano na ugonjwa huu wa Corona zoezi la kunawa mikono ni muhimu sana, tumekuwa tukiwahimisha wafanyakazi na wateja wetu, na sasa tunaungana na Chama cha Madaktari kuwahamasisha Watanzania kunawa mikono mara kwa mara au kutumia vitakasa mikono (hand sanitizer),” alisema Nsekela huku akimtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL, Waziri Kindamba kuungana naye kuwahamasisha Watanzania kunawa mikono katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

No comments:

Post a Comment

Pages