Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akitolea ufafanuzi hoja zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusiana na mradi wa ujenzi wa Maktaba ya
Chuo cha Ardhi Tabora wakati kamati hiyo ilipokwenda kukagua maendeleo ya mradi
huo mwishoni mwa wiki . Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati Kemilembe Lwota na
kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii Magdalena Sakaya akiwasilisha hoja kuhusiana na Mradi wa
ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora mwishoni mwa wiki wakati Kamati yake
ilipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.
Na Munir Shemweta, WANMM TABORA
Kamati ya Bunge ya Kudumu
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeamua kuubeba mradi wa ujenzi wa
Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora kilichopo mkoani Tabora kwa lengo la
kuhakikisha mradi huo unapatiwa fedha za kutosha na kukamilika ili kukiwezesha
chuo kuwa na Maktaba kubwa na ya kisasa.
Uamuzi huo wa Kamati
unafuatia kuelezwa kuwa, ujenzi wa mradi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora umeshindwa
kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya fedha pamoja na na majadiliano ya
muda mrefu kati chuo na Mshauri Msimamizi wa ujenzi ambaye ni Wakala Ujenzi
Tanzania (TBA).
Akizungumza mwishoni
mwa wiki mkoani Tabora wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na
Utalii ilipokwenda kukagua maendeleo ya mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati Kemilembe
Lwota alisema, kamati yake imeamua kuubeba mradi huo kama suala maalum na
kulipeleka mbele zaidi na kuhakikisha kama kamati wanaifanya kazi hiyo kwa
uhakika ili kusaidia kukamilika kwake.
‘’Hata hiki kizuri
kilichokuja cha kujenga maktaba mlichoanza kukitengeneza lakini ndani ya miaka
mitano ujenzi umesimama kweli kuna shida, naungana na wajumbe wenzangu hili
suala tutalichukua kama issue mahsusi ya kamati na tutalipeleka mbele zaidi na
kufanya kazi hiyo kwa uhakika na umakini zaidi’’ alisema Kemilembe.
Mbunge wa jimbo la
Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye ameshangazwa na mradi wa ujenzi wa maktaba hiyo
kutokamilika kwa wakati pamoja na kamati hiyo kusaidia mara kadhaa kujenga hoja
za kusaidia upatikanaji fedha. Ameitaka Serikali kuhakikisha fedha za ukamilishaji
ujenzi huo zinapatikana.
Naye Mbunge wa jimbo la
Kaliau mkoani Tabora Magdalena Sakaya alisema, pamoja na Tanzania kuwa na vyuo
vya ardhi viwili (Morogoro na Tabora) vinavyotoa wahitimu wa ngazi ya Cheti na Diploma
lakini kutokamilika kwa mradi wa Makataba ya Chuo hicho unachangia migogoro ya
ardhi inayosababishwa na ukosefu wataalamu wa kutosha katika fani mbalimbali za
ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwaeleza wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii kuwa, changamoto iliyosababisha
kutokamilika mradi wa ujenzi wa Maktaba ya chuo cha ardhi Tabora kwa wakati ni upatikanaji
mafungu ya fedha kutokuja kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo, Dkt Mabula alisema
pamoja na changamoto hiyo chuo kimeendelea kufanya vizuri katika utendaji kazi ikiwemo
kuongeza udahili kila mwaka na kubainisha kuwa katika jitihada za kukijengea
uwezo wa chuo Wizara imekipa mradi wa kuzalisha baadhi ya nyaraka zinazohusiana
na masuala ya ardhi.
No comments:
Post a Comment