NA
MWANDISHI WETU
KAMPUNI
Tigo Tanzania kwa kushirikiana na
Samsung Electronics wamezindua simu janja aina ya Samsung S20 nchini ambayo
ina ubora wa kimataifa.
Hayo
yamesemwa na Meneja wa Bidhaa za Untaneti wa Tigo, Mkumbo Muyonga akizungumza
wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema
“Ni jambo la kubwa sana kwetu kuchaguliwa na Samsung kuwa wa kwanza kuzihifadhi
na kuuza simu za Samsung S20 kwenye soko la Tanzania.
Hii
inaonesha imani yao kwetu juu ya mtandao mkubwa wa usambazaji tulionao na pia
kupitia timu yetu ya huduma kwa wateja inayotoa huduma zenye ubora wa hali ya
juu,”alisema Muyonga.
“Lengo letu ni kuchochea mageuzi ya kidigitali
katika maisha ya watu hapa nchini na ndio maana tumeungana na Samsung ili
kuongeza idadi ya umiliki wa simu janja pamoja na matumizi ya data ili
kuhakikisha watu wengi zaidi wanaifikiwa na teknolojia hii,” alisema Muyonga.
Muyonga
aliongeza “Tunalenga kuongeza ueneaji wa simu janja nchini huku tukihakikisha
wateja wetu wanafurahia huduma za kidigitali kupitia mtandao mkubwa wa 4G hapa
nchini.
Na
ndio maana tunatoa GB 78 za intaneti kwa mwaka mzima kwa wateja wote
watakaonununa Samsung Galaxy S20, S20+ na S20 Ultra,” alisema.
Alisema
ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuongea matumizi ya mtandao wa
4G na kuchangia ukuaji wa teknolojia ya kidigitali nchini.
Akizungumza
wakati wa uzindizu huo, Meneja wa
Samsung Tanzania, Suleiman Mohamed alisema Samsung imezindua simu ya Samsung
Galaxy S20 toleo jipya ulimwenguni ambayo itabadilisha namna ambavyo watu
wanavyoishi na kuufurahia ulimwengu.
“Galaxy
S20, S20+ na S20 Ultra ina camera ambayo ina uwezo wa kipekee wa kupiga picha
huku ikiwa na sifa mbalimbali ambazo zitamfanya mtumiaji kufurahia kuitumia
ikiwamo muziki,video zenye ubora pamoja na michezo (games) mbalimbali.
“Tukiwa
tunaingia kwenye muongo mwingine, kuna mabadiliko makubwa kwenye sekta ya
mawasiliano na namna watu wanavyo ujua na kuufurahia ulimwengu,” alisema.
Alisema
Samsung inahakikisha inatoa teknolojia na vifaa vya kisasa zaidi ili kuendana
na mabadiliko hayo kwa kutumia camera yenye mfumo wa AI unaweza kupata kila
tukio na kuungana na
No comments:
Post a Comment