HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 20, 2020

MSANII WA VICHEKESHO IDRIS SULTAN APANDISHWA KIZIMBANI

 Msanii wa vichekesho Idris Sultan, akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2020.



Na Mwandishi Wetu

MSANII wa vichekesho nchini, Idris Sultan na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na kosa moja la kuchapisha maudhui mtandaoni bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Doctor Ulimwengu na Isihaka Mwinyimvua ambapo wote kwa pamoja walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa makosa yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Wakili wa Serikali, Batlida Mushi.

Katika kesi hiyo namba 60 ya mwaka 2020, Wakili Mushi amedai kuwa Idris na wenzake wametendeka kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 12, 2020 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika maeneo hayo walirusha maudhui kupitia chaneli ya YouTube huku wakiwa hawana kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa wote walikana kitenda kosa hilo ambapo wakaachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja kwa kila mshitakiwa ambao wamesaini bondi ya Sh.Milioni nane kila mmoja.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyi hadi Aprili 21,2020 ambapo itarudi kwa ajili ya kusikilizwa.

No comments:

Post a Comment

Pages