Na Happiness Katabazi
MWANDISHI mkongwe wa Habari za michezo nchini, Asha Muhaji (pichani) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Asha ambaye aliwahi kuwa Msemaji wa timu ya Simba, enzi za uhai wake, nilipata fursa ya kufanya nae kazi katika baadhi ya vyombo vya habari yeye akiandika habari za michezo na mimi nikiandika habari ngumu (Hard News).
Taarifa za kifo cha Asha zilianza kusambaa kwa baadhi yetu waandishi wa habari saa 2 asubuhi leo kuwa amefariki taarifa ambazo tulikuja kuthibitisha zilikuwa ni uzushi na kwamba nikweli Muhaji alikuwa na hali mbaya na kalazwa chumba Cha wagonjwa mahututi (ICU) hospitalini hapo na ilipofika saa alasiri leo ndio waandishi wa habari wenzangu ambao wao Ni waandishi nguli wa habari za michezo Dina Ismail (Habari Leo) na Mwani Nyangasa.
February 10 mwaka huu, mimi Happiness, Mwani Nyangasa na aliyekuwa Msemaji wa TFF, ambaye kwa sasa Ni Mwanasheria mwenzangu Alfred Lucas tulikutana Sinza na tukabadilishana mawazo.
Katika mazungumzo yetu tulipanga siku moja tutenge tukamjulie hali Mwandishi mwenzetu Asha kwani alikuwa nyumbani akiugua lakini hadi umauti unamkuta leo hatukuweza kumuona kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu isipokuwa nilikuwa nikiwasiliana nae kwa simu.
Binafsi napenda kumuelezea marehemu Asha kuwa alikuwa Ni miongoni mwa waandishi wa habari wa kike wachache nchini ambayo waliitendea haki taaluma yao katika upande wa habari za michezo.
Asha alikuwa anavyanzo vingi vya habari za michezo(source) hasa ndani ya klabu ya Simba na klabu nyingine hali iliyokuwa inamsaidia kupata taarifa hata za klabu mbalimbali ambazo uongozi wa klabu inakuwa bado hazijazitoa taarifa hizo rasmi kwa umma.
Ikumbukwe Asha kabla ya kuwa Msemaji wa Simba alifanyakazi katika magazeti mbalimbali likiwemo gazeti Uhuru na Mtanzania ,Dimba.
Na hata alipomaliza mkataba wa kazi ya kuwa Msemaji wa Simba alirudi katika vyombo vya habari kuendelea na kazi yake uandishi wa Habari.
Asha kilichokuwa kinaniunganisha mimi na yeye ni alikuwa anapenda urembo, umaridadi na burudani na kupenda kucheka kama mimi. Hakika mbali na taaluma yetu ya uandishi wa habari vitu hivyo hasa ndiyo tulikuwa tunashare pamoja.
Yaani navuta kumbukumbu za enzi zile katika mabonanza ya waandishi wa habari yaliyokuwa yakifanyika Sine Club, Msasani Beach Club , TCC Chang'ombe, tulikuwa mstari wa mbele katika kuakikisha sherehe za mabonanza ya waandishi na alipenda.
Kifo chako Asha ambaye ulikuwa unashabikia Simba mimi nashabikia Yanga. kimeniuma.
Utakumbukwa na mashabiki wenzako wa Simba, waandishi wa habari wenzako, mchango wako katika tasnia ya uandishi wa habari tutauenzi kwa sababu umeacha alama katika fani.
Sisi tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
Mungu aiweke roho ya mwanahabari mwenzangu Asha Muhaji mahali panapostahili. Amina.
Mwandishi wa makala hii ni Mwandishi wa habari na Wakili wa Kujitegemea.
0716 774494.
25/3/2020.

No comments:
Post a Comment