HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 26, 2020

Kanisa Ladaiwa Kodi ya Ardhi SH. Bil.1.2

Mkuu  wa Kitengo cha Kodi  Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, Denis Masami  akizungumza nje ya Kanisa Anglikana Mtakatifu Bernard Buza jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kuwafuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango ya ardhi.

Na Asha Mwakyonde

MKUU  wa Kitengo cha Kodi  Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi Denis Masami amessma kuwa Kanisa Anglikana  Mtakatifu Bernard Buza jijini Dar es Salaam linadaiwa  kodi ya ya shamba lenye ukubwa wa hekari 410 kiasi cha  bil.1.200  tangu mwaka 2005 hadi sasa.

Amesema awali Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi pamoja na Manispaa ya Temeke  waliupelekea hati ya madai uongozi wa kanisa hilo

Akizungumza jijini Dar es Salaam  Machi  25, mwaka huu katika ziara ya kuwafuatilia wadaiwa sugu wa kodi za pango ya ardhi, Masami amesema  kanisa hilo limefunja masharti ya uendelezwaji wa eneo hilo.

Masami amesema kuwa uongozi wa kanisa hilo unafanya biashara kwa kutumia mwavuli wa kanisa na kwamba asilimia 90 wa uendelezwaji wa eneo hilo ni Viwanda.

Amesema taasisi hiyo ya kidini inafanya biashara eneo la kanisa ambapo imepangisha wafanyabiasha wa maduka zaidi ya 200, viwabda, nyumba za kuishi  kituo cha mafuta cha Lake Oil Buza huku uongozi huo  ukichukua kodi bila kulipa panga la ardhi.

" Tungeweza kuweka kadi  hii ya viwanda taasisi ingedaiwa zaidi ya bil.5 hiki kiasi cha bil.1.200 ni kodi ya pango ya ardhi  ni kuipotezea serikali mapato," amesema Masami.

Mkuu huyo wa kitengo anaongeza kuwa eneo la kanisa  halizidi upana wa mita 50 lakini maaeneo  yote ni viwanda  na kwamba hakuna sababu ya kanisa hilo kuendelea kulipa kodi ya shamba.

Aidha ametoa rai kwa Ofisa mipango  miji ahakikishe  wanafanya marekebisho  na kuwatoza  faini pamoja na kubadilisha  matumizi eneo hilo ili walipe kodi stahiki.

Katika hali ya kushangaza  uongozi wa kanisa hilo ulikwepa kuongea na mkuu huyo  alipotaka kujua ubalishwaji wa matumizi wa eneo husika.

Ametoa wito kwa taasisi zote za Umma na za kidini ambazo zinatumia ardhi kibiashara  kulipa kodi ya pango ya ardhi.

Naye Ofisa ardhi Wilaya ya Temeke Erick Asenga amesema kuwa kuanzi Machi 30 mwaka huu wale wote  waliokiuka maagizo  ya kulipa kodi ya ardhi atawapelekea hati ya madai  na kuanza kuwafuatilia.

"Tunawasihi wale wote waliopelekewa hati ya madaj waanze kulipa kwa wakati ili kuepuka mkono wa sheria," amesema Asenga.

Amesema  kuwa uongozi wa Kituo  mafuta cha Lake Oil  Buza  wameahidi kupekeka mkataba wao katika Manispaa ya Temeke ili uwezwe kuangalia  na kujua aliyewapangisha.

No comments:

Post a Comment

Pages