Washington, Marekani
Tanzania
na Benki ya Dunia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala
mbalimbali ikiwemo elimu,uendelezaji wa miundo mbinu na masuala ya
kijamii kupitia mikopo,ruzuku na misaada inayotolewa na benki hiyo ili
kuisaidia Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo na kutokomeza umasikini
miongoni mwa raia wake.
Hayo
yamebainika baada ya mazungumzo baina ya Mkurugenzi mtendaji wa benki
ya Dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer "DJ" Nordquist na Mjumbe
maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki hiyo
Washington Marekani ambapo wamejadili masuala mbalimbali hususani kuhusu
masuala ya mahusiano baina ya Benki ya dunia,Marekani na Tanzania.
Pia
wamezungumzia masuala mbalimbali ya miradi maendeleo ikiwa pamoja na
sekta ya elimu na kujadili maeneo mbalimbali ambayo Benki hiyo
imeisaidia Tanzania aidha kwa mikopo ya masharti nafuu au misaada ikiwa
ni pamoja na ujenzi na uendelezaji wa shule za msingi na sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer "DJ" Nordquist amesema
anafuatilia kwa ukaribu masuala yote yanayoendelea Tanzania na kwamba
anavutiwa na mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika utoaji wa elimu
bure kwa shule za msingi na sekondari.
Aidha Dkt Jennifer "DJ" Nordquist ameeleza
kufurahishwa kwake na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali na
kusisitiza kuwa ni vyema elimu inayotolewa isiwe na ubaguzi na kuahidi
kuendelea kushirikiana na Tanzania kuoata fedha ziatakazowezesha
kuboresha miundombinu ya elimu nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa mabweni katika shule za kata na kutoa mfumo maalum wa utoaji wa
elimu kwa wanafunzi wanaokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali
ikiwa ni pamoja na wale wanaopata ujauzito.
Mkurugenzi
Mtendaji mbadala wa Kanda Namba 1 ya Afrika kutoka Benki ya Dunia Bw.
Taufila Nyamadzabo amesema mazungumzo baina ya Tanzaia na benki ya dunia
yamekuwa ni ya manufaa kwa kuwa yameondoa sintofahamu iliyokuwepo kati
ya pande hizo mbili na ni matumaini yake mradi huo utapitishwa na bodi
ya benki ya dunia hivi karibuni.
Katika
tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharki
Prof. Palamagamba John Kabudi amewasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kweda kwa
Rais wa Marekani Mhe. Donald Trump kupitia Wizara ya mambo ya Nje ya
Marekani.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye pia anashughulikia masuala ya
Afrika Mhe. Tibor Nagy ndiye aliyepokea ujumbe huo na kuahidi
kuendeleza mashirikiano mazuri nay a muda mrefu yaliyopo kati ya
Tanzania na Marekani. Katika mazungumzo hayo Naibu Waziri huyo
ameambatana na Balozi Mteule wa Marekani Nchini Tanzania Dkt. Donald
Wright
No comments:
Post a Comment