Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akitoa
ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha
kujadili taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2019/20
na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2020/21 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Kituo
cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya
Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.
Cosmas Ngangaji akiwasilisha taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa
Bajeti wa Mwaka 2019/20 na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2020/21 kwenye Kikao cha
Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Kituo
cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment