Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mamia ya watu wenye ulemavu kwenye matembezi ya hiari kumuezi Muasisi wa Taasisi ya Dk. Regnald Mengi kwa Watu wenye Ulemavu (DRMF), kuhitimisha mwezi wa kumbukizi ya matendo ya huruma aliyoyafanya Dk. Mengi enzi za uhai
wake.
Matembezi hayo yatafanyika Mei 31 kuhitimisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupanda miti kulinda vyanzo vya maji, kuchangia damu na michezo jumuishi kwa wenye ulemavu zitakazoanza kufanyika Mei Mosi mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyolewa na Mkurugenzi wa taasisi ya DRMF, Shimimana Ntuyabaliwe, ilibainisha kwamba Mei ni mwezi wenye matukio matatu muhimu kwa hayati Dk. Mengi hivyo lazima kufanya mambo
aliyopenda kuyafanya enzi za uhai wake hasa shughuli zinazowahusu walemavu.
“Mei ni mwezi muhimu kwetu kwa sababu umebeba matukio matatu… kwanza ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu muasisi wetu afariki dunia Mei 2,2019 tarehe 18 ndipo taasisi yetu iliposajiliwa rasmi na Mei 29 ni siku ya kuzaliwa kwa Dk. Mengi hivyo tuna kila sababu ya kuuheshimu na
kufanya matukio ya kumuenzi,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Ilieleza kwamba DRMF kwa kushirikiana na Jakaya Kikwete Youth Park na COPE, wameandaa michezo mbalimbali ya walemavu iliyopewa jina la ‘Tembea kwenye viatu vyangu’ yenye lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam, kutambua changamoto za walemavu.
“Mei 7 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu atazindua michezo hiyo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park ambapo wanafunzi zaidi ya 1,000 kutoka shule mbalimbali za msingi watashiriki.
“Mei 8 watumishi wa taasisi yetu, watanzania wengi pia wanakaribishwa na wadau wa afya ambapo ptutachangia damu kwenye viwanja vya Mbagala Zakeem tukiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu… tunawaomba watanzania wajitokeze kwenye jambo hili muhimu la kuokoa maisha ya wenzetu,” ilisomeka sehemu ya taarifa ya Ntuyabaliwe.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo shughuli nyingine zitakazofanywa na taasisi hiyo kumuenzi Dk. Mengi ni kupanda miti na kuwahamasisha watanzani wengine wafanye hivyo kwenye maeneo yao ili kulinda vyanzo vya maji, uoto wa asili na kujikinga na mabadiliko hasi ya tabianchi.
“Enzi za uhai wake Dk. Mengi alipanda miti milioni 24 pembezoni mwa Mlima Kilimanjaro. Sisi tutapanda miti kwenye Makao Makuu ya nchi, jijini Dodoma Mei 12 tukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Zungu na Mei 29 tutapanda tena miti kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla.”
Ntuyabaliwe aliwaomba watanzani hasa wenye ulemavu kuutumia mwezi huo kumuenzi Dk. Mengi na kuisaidia jamii kwenye maeneo tofauti aliyopenda kufanya enzi za uhai wake.

No comments:
Post a Comment