Mshindi kwa Watoto Karim Ismail akipokea zawadi ya baiskeli kutoka kwa moja ya wadhamini Brenda Dickson wakati wa ufungaji mashindano ya Tanapa Lugalo Open kwa mwaka 2020 katika Hafla iliyofanyika jana Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Na Luteni Selemani Semunyu
Waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo
Dr Harrison Mwakyembe amesema Serikali itahakikisha inatafuta ufumbuzi wa
changamoto wa Uhaba na Ubovu wa viwanja Vya Mchezo wa Golf hapa Nchini na
kuliomba Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kusaidia kukabiliana na
Changamoto hiyo.
Wazirii Mwakyembe alisema hayo jana wakati
akifunga mashindano ya mchezo wa gofu ya TANAPA Lugalo Open yaliyofanyika katika Viwanja vya Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania vya Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mwakyembe alisema mchezo wa gofu umekua
na changamoto nyingi hasa ya ubovu na uchache wa miundombinu ya viwanja hivyo
serikali itahakikisha changamoto hizo zinatafutiwa ufumbuzi kwa kushirikiana na
wadau wa sekta ya michezo.
“Natoa rai kwa wadau mbalimbali wa michezo
kuwekeza kwenye mchezo wa gofu ili kuuendeleza mchezo huo nalipongeza Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imekuwa Chachu yaa Kuendleza Mchezo huu na
kuvipa nguvu Vyma vya Golf kwa Kuwapa Ofisi “ Alisema Dk Mwakyembe.
Pia Waziri Mwakyembe ametoa wito kwa
wadhamini wakuu wa mashindano hayo ambao ni Tanapa kuendelea kudhamini mchezo
wa kwani mchezo huo unanafasi kubwa katika kuutangaza utalii wa nchi na Taifa
kwa Ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya gofu
Lugalo Brigedia Jeneral Mstaafu Michael Luwongo amemuomba Waziri Mwakyembe
kupitia wizara yake kuupa kipaumbele na kuutangaza mchezo wa gofu ili Tanzania
itambulike kimataifa kupitia mchezo wa huo kutokana na michezo mingi hapa
nchini kutangazwa zaidi.
Nae Mwakilishi wa TANAPA Hassan Ngulume
ambao wamedhamini mashindano hayo alisema
wameshukuru kwa kupata nafasi ya kudhamini Golf na kuahidi kuendelea
kutoa udhamini ili kuongeza uelewa wa hifadhi kwa watalii hasa wa ndani.
Kwa upande wa matokeo ya mashindano hayo
mchezaji Victor Joseph wa klabu ya Dar es salaam gymkhana ameibuka na ushindi
baada ya kupiga mikwaju 153 wakati
mshindi wa jumla aliyepiga Mikwaju ya Jumla Net 142 ni Godfrey Abel.
Wakati Katika Divisheni B Mshindi ni Fabian Magoti aliyepiga mikwaju ya Jumla 143
huku Mshindi wa Pili ni Zakaria Edward aliyepiga mikwaju ya Jumla 148 wakati
Divisheni B Mshindi ni John Hiza wa
Lugalo kwa Mikwaju ya Jumla 143 akifuatiwa na
Teddy kalinga kwa Mikwaju ya Jumla 145.
Divisheni C Mshindi ni Nathaniel Ayonga wa
Lugalo Kwa Mikwaju ya Jumla 148
akifuatiwa na Laurent Sangawe naye wa
Lugalo kwa Net ya 150 huku kwa Wanawake Mshindi ni Angel Eaton kwa mikwaju 159 bada ya kufungana mshindi kwa wanawake kwa
mikwaju ya jumla 147 ni Hawa Wanyenche.
Mshindi wa wa pili kwa wanawake kwa mikwaju
ya jumla 151 ni Ayne Magombe wakati
mshindi kwa wazee ni Jin Soo Yang
aliyepiga mikwaju ya jumla 151 na kufuatiwa na Dk Edmund Mdolwa aliyepiga mikwaju ya jumla 152
Kwa upande wa watoto mshindi kwa kwanza ni
Karim Ismail aliyepiga Mikwaju ya jumla
69 akifuatiwa na Hamad Maulid aliyepiga mikwaju ya jumla 70.
No comments:
Post a Comment