Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amewataka wakazi wa Wilaya hiyo
kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Vizuri vya Corona ikiwa ni
pamoja na kupokea wageni wasio wajuwa bila kuwa na uhakika wa afya zao.
Mhe.
Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa kwenye mkutano na wananchi uliokuwa na lengo la
kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa
mwenzake sambamba na kuepuka kukaribisha wageni kienyeji.
Ameongeza kuwa
“ kuanzia leo nyinyi wenyewe muwe walinzi wa wenzenu, chukueni tahadhari, msije
kupokea wageni wa aina yoyote ile kwa sababu wapo watu ambao wanaweza kutumia
njia mbalimbali za kuleta vizuri hivyo katika maeneo yetu” amesisitiza Mhe.
Chongolo.
Katika hatua
nyingine Mhe. Chongolo amezindua Bandari Bubu iliyopo Mbweni nakuzitaka Malaka za Mapato Tanzania (TRA),
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuepusha
changamoto kwa wananchi, wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo.
Mhe.Chongolo
amesema kila mamlaka husika zinapaswa kuwepo katika eneo pamoja na Taasisi
nyingine ili kuwezesha wananchi na wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo
kufanya shuguli zao kwa urahisi kulingana na mazingira rafiki yaliyopo.
Amefafanua kuwa
Nchi ilikuwa inakosa mapato mengi kupitia upitishaji wa magendo katika maeneo
ya fukwe za Mbeni, Ununio, Kunduchi pamoja na maeneo mengine ya pembezoni mwa
fukwe za bahari na hivyo kueleza kuwa tayari bandari hiyo imeruhusiwa kutumika
na watu kufanyabishara zao.
”hapo awali tulikuwa hatupati fedha kwenye hii
Bandari, ila hivi sasa tumeanza kupata fedha , naomba tushirikiane vizuri na nikiondoka
hapa kwenye mkutano , mamlaka zote ambazo zinapaswa kuwepo hapa ziwepo ikiwemo TRA,
tunataka mapato wao wasiwe kikwazo cha kutukosesha mapato.
Katika hatua
nyingine Mhe. Chongolo amemtaka OCD wa Kawe kuhakikisha kuwa usalama kwa
wafanyabiashara unakuwepo sambamba na kuwachukulia hatua wote ambao watakiuka
na kushindwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.
No comments:
Post a Comment