HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2020

Zaidi ya Laini Milioni 35 zasajiliwa kwa alama za Vidole-Mhandisi James Kilaba

*TCRA yataja mafanikio ya usajili wa Alama za Vidole
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza katika Siku ya Walaji ambayo huadhimishwa kila Machi 15 Duniani ya kila mwaka.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Fredrick Ntobi akitoa maelezo kuhusiana na maadhinisho ya Siku ya Walaji ambayo huadhimishwa kila Machi 15 ya Kila Mwaka Mkutano uliofanyika makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.

 
Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini(TCRA) imesema  jumla ya laini 35,813,455 kati ya 43,072,868 zilizounganishwa  mitandano zimeshajiliwa kwa  alama za vidole  mpaka kufikia Machi 10 mwaka  huu.

Akizungumza jana  wakati wa maazimisho ya  Siku ya Haki ya Mlaji  Duniani Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema kuwa idadi  hiyo ambayo ni sawa na asilimia 83.1 ya  laini zote    ni wazi kuwa zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole limekuwa na manufaa.

“TCRA  mpango wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole mnamo 2018,zoezi hili limekuwa na  manufaa  na kupata mwitiko mkubwa ambapo hadi kufikia Machi 10,2020 idadi ya laini zilizounganishwa  mitandanoni ni 43,072,868 huku idadi ya laini zilizosajiliwa  kwa alama za vidole ni 35,813,455 sawa na asilimia 83.1 ya laini zote,”alisema Mhandisi Kilaba.

Amesema lengo la usajili wa kutumia mfumo huo ni kuimarisha usalama katika matumizi ya simu za mkononi ,kulinda watumiaji na kufanikisha shughuli nyingine za usimamizi.

Amesema wakati watumiaji wakiadhimisha siku ya mlaji ni muhimu wakakumbuka wajibu wa kila mmoja kusajili laini yake ya simu kwa mfumo  wa  kutumia alama za vidole ambapo  kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa nchini(NIDA).

Akizungumzia kuhusu siku ya Haki ya Mteja Duniani Mhandisi Kilaba alisema siku hiyo huadhimishwa kila  mwaka Machi 15 kila mwaka ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Mteja Endelevu’.

“Kauli mbiu inajikita katika kusisitiza umuhimu wa upatikanaji wa huduma endelevu nasi katika sekta ya mawasiliano tumekuwa tukilitekeleza hilo,tunalitekeleza  na tutaendelea kulitekeleza wakati wote,”alisema Mhandisi Kilaba.

Amesema   katika maadhimisho haya TCRA imekuwa ikifanya mikutano mbalimbali na wadau kwa muda wa wiki  nzima  wakitoa elimu ya mawasiliano katika shule na vyuo mbalimbali katika mikoa ya Shinyanga,Tabora,Arusha,Zanziba na Pwani.

No comments:

Post a Comment

Pages