HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2020

RC TABORA AAGIZA WATOTO WANAOZURURA KUCHUKULIWA HATUA

Na Tiganya Vincent

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza viongozi wa Halmashauri mbalimbali kuanza kuchukua hatua dhidi ya watoto wote wanaodhurura ovyo mitaani na kuhatarisha maisha yao baada ya shule kuwa zimefungua kwa ajili ya kuwakinga na Corona.

Alisema haiwezekani Serikali ilifunga Shule kwa ajili ya kuwaondoa watoto katika msongamano bado kuwa baadhi yao wanaonekana katika mitaa wakiuza karanga, mchicha na wengine wakiwasaidia wazazi wao kuuza chakula katika migahawa ya chakula.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati kipindi maalumu cha kuwaelimisha wawakilishi wa watu wenye ulemavu jinsi ya kukabiliana na janga la Corona ambalo kilikuwa pia kikitangwa na redio za Kijamii mkoani hapa.

Alisema watoto wanatakiwa kukaa majumbani huku wakifuatilia masomo kwa njia ya vyombo vya habari na wengine wakipitia vitabu mbalimbali ili kujikumbusha walichofundishwa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema pindi janga la Corona litakapokuwa limemalizika na Shule kufunguliwa wanafunzi wote wa kike ni lazima wapimwe ujauzito baada ya kuwekuwepo na tuhuma kuwa baadhi yao wameonekana katika maeneo ya nyumba za kulala wageni.

Alisema watakaobainika kuwa na ujauzito watachukuliwa hatua kali ikiwemo wazazi wao na mtu atakayekuwa akituhumia kumrubuni na kumpa ujauzito.

Mwanri aliwataka wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki ambacho hawako shuleni ili kuwalea katika maadili mema.

Awali Mratibu wa Wajasiriamali Mkoa wa Tabora Ashura Mwanzembe alisema baadhi ya watoto wa kike wamekuwa wakitumika kuuza karanga, mahindi ya kupika kuingia katika nyumba za kulala wageni kwa madai ya kutafuta wateja wa bidhaa wanauza huku wakijiweka katika hatari.

Alisema hivi karibuni alilazimika kumchapa binti mmoja aliyekuwa akiuza karanga baada ya kumuona akitoka katika nyumba ya kulala wageni kwa kisingizio kuwa alikuwa akitembeza karanga ndani.

Ashura aliwaomba wazazi kuacha kuwafanyisha kazi za kuuza mchicha , karanga na vitu vingine kwa kuwa watu wenye nia mbaya wamekuwa wakiwarubuni kwa kujifanya wananunua vitu vyote kwa mkupuo kwa niaba kuwataka kimapenzi huku wanawaharibia maisha.
 Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipa elimu ya kujikinga na Corona kutoka kwa wataalamu na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi jana kwa watu wenye ulemavu wakati wa muendeleza wa utoaji wa elimu ya kujinga na Corona kwa makundi mbalimbali Mkoani humo. Elimu hiyo ilikuwa ikirushwa na Redio mbalimbali za Mkoa huo. (Picha na Tiganya Vincent).

No comments:

Post a Comment

Pages