Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mahenge mara baada ya kufanya
ziara ya kuwasikiliza na kujionea athari zilizosababishwa na wanyamapori
wakali na waharibifu walivyoharibu mazao katika mashamba ya Wananchi
hao katika mkutano uliofanyika katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo, Mwajuma
Nasombe kabla ya kuanza kuzungumza na wananchi wa Kata ya Lugalo
kufuatia makundi ya Simba yaliyovamia Kata hiyo na kula ng'ombe wawili
wa mkazi wa Kata hiyo Bw.Aloyce Nziku.
Naibu
Waziri wa Malasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa ameongozana
na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuzungumza na
wananchi wa Kata ya Lugalo iliyopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
kufuatia kuvamiwa na makundi ya Simba ambayo yalikula ng'ombe wawili wa
mkazi wa Kata hiyo Bw.Aloyce Nziku ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka
wananchi watoe taarifa mapema wanapovamiwa na Wanyamapori.
Mbunge wa Kilolo, Mhe. Venance Mwamoto akisalimiana na Mchungaji kwa
kugonga miguu ikiwa ni salamu inayoshauriwa kutumiwa kwa sasa kutokana
na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ili kuepuka kuambukizana virusi vya
ugonjwa huo
mara baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine
Kanyasu kumaliza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Irindi kilichopo
katika wilya ya Kilolo mkoani Iring.
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema sekta ya
Utalii nchini inapitia katika kipindi kigumu sana tangu nchi ipate Uhuru.
Amesema
kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona kuanzia mwezi Februari mwaka
huu idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vya Utalii nchini imezidi
kupungua hadi kufikia hakuna Mtalii kabisa.
Ametoa
kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya
Irindi, Ikula, Lugalo na Mahenge katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
wakati alipofanya ziara ya kikazi ya Siku moja ya kutembelea kujionea
uharibifu wa mazao uliofanywa na wanyama wakali na waharibifu katika
mashamba ya wanavijiji hao.
Mhe.Kanyasu
amesema tangu ugonjwa huo kuanza Sekta hiyo ambayo kwa zaidi asilimia
95 hutegemea watalii wa kutoka nje za nchi kuja kutembelea vivutio vya
utalii imeathirika sana kimapato.
Akizitaja
Taasisi za Uhifadhi nchini zilizoathirika na mlipuko wa virusi vya
Corona ikiwemo Shirika la Hifadhi Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi
Ngorogoro, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania pamoja Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania.
Amesema
watalii wengi kutoka Nchi za nje baada ya kutokea ugojwa huo watalii
wengi waliokuwa wamepanga kuja nchini waliahirisha safari zao huku
wengine walizifuta kabisa.
Hata
hivyo, Mhe.Kanyasu ametoa wito kwa watalii waliokuwa wamepanga
kutembelea vivutio vya utalii nchini wasizifute safari zao badala yake
waziahirishe ili baada ya ugonjwa huu kuisha waweze kuja.
Akizungumzia
athari za utalii nchini Tanzania, Mhe.Kanyasu amesema ugonjwa huo
umesababisha hoteli za kitalii zilizopo katika Hifadhi zote nchini
kufungwa kwa vile hakuna watalii wanaokwenda kutalii
Aidha, Amesema hoteli kubwa zilizo katika miji kavile Dar es Salaam, Kilimanjaro pamoja na Arusha zimefungwa kwa kukosa watalii.
Amesema
kuibuka kwa ugonjwa huo kumpelekea Mashirika ya ndege Duniani kusitisha
kutoa huduma za usafiri kwa hofu ya kusambaza zaidi ugonjwa huo kwa
idadi kubwa ya watu hivyo sekta ya utalii imezidi kusinyaa siku hadi
siku
Mbali na athari
hizo, Mhe.Kanyasu amesema kusinyaa kwa sekta ya utalii ambayo imekuwa
ikichangia asilimia 17 ya pato la Taifa imepelekea idadi kubwa ya watu
kukosa ajira.
Katika
hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi wote kuchukua tahadhari
juu ya virusi vya Corona kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu ipasavyo
Aamewataka kuhakikisha hawapeani salamu kwa kushikana mikono pamoja na kuhakikisha wananawa mikono pale inapohitajika.
Kwa
upande wake Mbunge wa Kilolo, Mhe.Venance Mwamoto amewataka wananchi
walioharibiwa mazao yao na wanyama wakali na waharibifu wawe watalivu
Serikali inayafanyia kazi maombi yao.
No comments:
Post a Comment