Dodoma, Tanzania
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Viongozi wa madhehebu ya Dini nchini, imeandaa maombi maalum
Kitaifa kuiombea Nchi dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayotokana na
Virusi vya Corona.
Maombi hayo yatakayoongozwa na Viongozi Wakuu wa
madhehebu ya Dini nchini, yatafanyika Jumatano tarehe 22 Aprili, 2020 katika
Viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam, kuanzia Saa 3.00 Asubuhi ambapo
Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Hatua hii ni utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa viongozi wa
Dini na Serikali uliofanyika tarehe 9 Aprili, 2020 Jijini Dar Es Salaam kuwa
yafanyike maombi ya kitaifa yanayojumuisha madhehebu yote nchini kuomba dhidi
maambukizi ya Corona.
Aidha, maombi haya ni mwendelezo wa maombi ya siku tatu
mfululizo yaliyotangazwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia tarehe
17-19 Aprili, 2020.
Viongozi wachache watahudhuria maombi haya kuwakilisha wananchi
ikiwa ni katika hali ya kuchukua tahadhari ya maambukizi hivyo, wananchi
mnasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kufuatilia maombi
haya mkiwa katika maeneo yenu kupitia vyombo mbalimbali vya
habari.
JIKINGE, WAKINGE WENGINE CORONA INAZUILIKA.
No comments:
Post a Comment