HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2020

TYEC MKOA WA SINGIDA YATOA ELIMU STENDI YA MABASI NAMNA YA KUJIKINGA KUPATA VIRUSI VYA CORONA

Mratibu wa Kamati ya Programu ya mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kutoka TYEC Mkoa wa Singida, Stella Mwagowa (kulia) akitoa elimu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Corona kwa Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na wafanyakazi wa mabasi katika stendi kuu ya mabasi mkoani hapa. 
Macmillan Marco, kutoka TYEC  akitoa elimu hiyo kwa abiria ndani ya basi.
 Mmoja wa Wanajumuiya ya TYEC, Richard  Assey, akionesha namna ya kujipaka Sanitizer kwa ajili ya kujikinga na Virusi vya Corona.
 Baadhi ya Vijana kutoka TYEC wanaojitolea  kutoa elimu  ya mapambano dhidi ya kuenea kwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona wakitoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara walio na vibanda vyao kuzunguka Stendi ya Mabasi mkoani hapa.
Mratibu wa Kamati ya Programu ya mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kutoka TYEC Mkoa wa Singida, Stella Mwagowa, akionesha jinsi ya kunawa ili kujikinga na Virusi vya Corona.
Afisa wa Polisi, Rashid Mirambo, akitoa elimu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Corona kwa . Kushoto ni Mwenyekiti wa TYEC, Mkoa wa Singida, Stanley Roman.
Macmillan Marco (kulia) kutoka TYEC  akitoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara waliopo stendi ya mabasi mkoani hapa.
Elimu ya kujikinga na Virusi vya Corona ikiendelea kutolewa.
TYEC wakijadiliana baada ya kutoa elimu hiyo stendi ya mabasi mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

Pages