Serikali
imesema licha ya mipaka ya nchi kujifunga kutokana na janga la ugonjwa
wa COVID 19,wageni wachache wanaoingia nchini wanapokelewa kwa mujibu na
taratibu za kuingia nchini na kuhudumiwa kwa hadhi inayoendana na
mahitaji ya Kimataifa kama ilivyo katika nchi nyingine yeyote duniani
huku tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo ikipewa kipaumbele.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi
Kanali Wilbert Augustine Ibuge ameyasema hayo alipofanya ziara katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua na kujionea namna
wageni kutoka mataifa mbalimbali wanavyopokelewa na hatua wanazopaswa
kuzifuata kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.
Balozi
Kanali Ibuge amesema licha ya ukweli kwamba kwa sasa wageni wanaoingia
nchini ni wachache sana kutokana na mipaka kujifunga ni muhimu serikali
kuhakikisha kuwa wale wachache wanaoingia wanafuata taratibu za nchi na
kupewa utaratibu wa namna ya kujikinga na ugnjwa wa COVID 19 bila ya
uwepo wa malalamiko kutoka kwa wageni hao.
Ameongeza
kuwa ameridhishwa na hali ilivyo katika uwanja huo wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere kwa kuwa hadhi wanayopewa wageni hao haina
tofauti na hatua zinazochukuliwa katika mataifa mengine duniani na
kwamba ni muhimu kufanya hivyo ili kuhakikisha usalama wa Taifa na raia
wake kwa ujumla.
Amewataa
watumishi wanaoendelea kutoa huduma katika uwanja huo kuchukua
tahadhari ya kujikinga na COVID 19 huku wakitumia kauli nzuri wakati wa
kutoa huduma.
Katika
ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Balozi Kanali Wilbert Ibuge amekagua jengo la kwanza la uwanja
huo na jengo jipya la tatu akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya
viwanja vya ndege TAA Mhandisi Julius Ndyamukama.
No comments:
Post a Comment