HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2020

NABII JOSHUA: TUTAHAKIKISHA CORONA INAONDOKA TANZANIA KUPITIA MAOMBI NA ELIMU KWA WATANZANIA WOTE

Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Joshua Mwantyala.
 
 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro

KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania,Nabii Joshua Aram Mwantyala amesema katika ibada ya Sikukuu ya Pasaka ambayo itafanyika Jumapili hii anatarajia kugawa vifaa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19).

Hatua ambayo itaenda sambamba na elimu juu ya namna ya kuchukua tahadhari ambayo inatarajia kutolewa na wataalamu wa afya kutoka mkoani humo. "Kwa umoja wetu wa maombi na kupitia elimu, tutahakikisha Corona inaondoka nchini Tanzania".

Nabii Joshua alisema, zoezi hilo pia litaenda sambamba na mfululizo wa maombi ya siku 40 ambayo yanalenga kuviondoa virusi hivyo katika uso wa Dunia.

Mbali na hayo amesema ataongoza maombi maalumu kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasaidizi wake kutokana na moyo wa unyenyekevu alionao kwa Mungu.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amezuia semina za serikali na mikutano ya kisiasa ikiwemo mikusanyiko isiyokuwa na sababu kwa sababu ya corona,lakini hajazuia ibada na mikutano ya kumuabudu Mungu. Hakika kupitia maombi yetu Mungu ataenda kumbariki na kumzidishia hekima na maarifa zaidi.

"Ni viongozi wachache sana wenye moyo wa namna yake, tena inawezekana duniani kote hayupo kwa sasa, kuwa na Rais anayetambua na kuthamini matendo makuu ya Mungu ni jambo la baraka sana;

Nabii Joshua aliyasema hayo mjini Morogoro wakati akiungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya namna walivyojipanga katika ibada ya Aprili 12, mwaka huu ambayo inatarajiwa kuwa ya kipekee kwa kila mmoja atakayeshiriki.

"Pia wakati nikiendelea na maombi nami nimeona niwe sehemu ya kuwabariki wale ambao hawana uwezo kwa ajili ya kununulia mahitaji ili kuweza kunawa mikono kama wanavyoelekeza wataalamu wa afya, kunawa mikono ni miongoni mwa hatua muhimu mno katika kujiadhari dhidi ya virusi vya corona, hivyo kadri Mungu atakavyonibariki, nami nitawabariki hivyo hivyo,lakini ninaamini Mungu anakwenda kuviondoa virusi hivyo katika uso wa Dunia siku si nyingi,"alisema Nabii Joshua.

"Hivyo kila mmoja afike ili akapokee uponyaji wake, pamoja na kupokea hizo baraka za kipekee,"alifafanua Nabii Joshua.

No comments:

Post a Comment

Pages