Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kuchakata mafuta ya Alizeti cha Yaza Investment kilichopo Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Yusuph Nalompa, akijiandaa kutoa taarifa kwa Waziri wa wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki.
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki amesikitika kuona Kiwanda cha kuchakata mafuta ya alizeti cha Yaza Investment kilichopo Wilaya ya Iramba mkoani Singida chenye uwekezaji mkubwa wa zaidi ya bilioni 10.2 kikiwa hakifanyi kazi licha ya miundombinu yake yote ikiwa imekamilika.
Waziri Kairuki alitoa masikitiko yake jana wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kutembelea miradi ya uwekezaji mkoani hapo ambapo alikagua viwanda vitano vya Yaza Investment, Kiwanda cha Singida Grains and Oil Mills au Singida Fresh, Kiwanda cha Meru Millers Ltd, Kiwanda cha Biosustain Tz Ltd na Kiwanda cha Q-STEK Tz Ltd.
Kairuki alisema kiwanda hicho kilitegemea kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 50 huku ajira zisizo za moja kwa moja zaidi 1000, kuzalisha mbegu, pamoja na wasafirishaji.
”Jambo ili linaumiza sana moyo na kusikitisha.” alisema Kairuki.
Alisema Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji imekuwa ikihimiza mara kwa mara kama juu ya uwekezaji kama ambavyo Waziri Mkuu mwenye wizara hiyo amekuwa akiweka mkazo katika kilimo cha mazao mkakati na hivi karibuni alionekana mkoani Kigoma akigawa miche ya mbegu za michikichi takriban milioni 1.8.
Alisema amekuwa akifanya hivyo sehemu mbalimbali lengo likiwa ni kuona Taifa linajitosheleza katika mafuta ya kula kwani kwa sasa tunaagiza mafuta hayo zaidi ya asilimia 60.
Kairuki alisema Mkoa wa Singida umejaaliwa na kuwa una baraka kwani zao la alizeti linastawi vizuri na kuwa Kiwanda cha Yaza Investment ni moja ya kiwanda kikubwa katika Wilaya ya Iramba na mwekezaji ni mzawa hivyo haitawezekana uwekezaji huo hupotee hivi hivi.
Alisema wizara inahimiza kuwepo na viwanda vingi vya kuzalisha mafuta ya kula na kuwa kama Taifa zaidi ya sh.bilioni 443 tunapoteza kwa ajili ya kuagiza mafutà na ukiangalia katika zao la alizeti zaidi ya asilimia 70 kwenye mafuta yanatokana na zao hilo hivyo ni lazima likapewa kipaumbele.
Aidha mempongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida na viongozi wengine wa mkoa huo kwa kuhimiza uwekezaji hususani wa viwanda vya uzalishaji wa mafuta ya kula ya alizeti.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho cha kuchakata mafuta ya alizeti cha Yaza Investment kilichopo wilaya ya Iramba, Yusuph Nalompa alisema yeye ni mfanyabiashara wa muda mrefu na kupitia kiwanda chake alikuwa akitoa ajira kwa vijana na kuongeza pato la Taifa.
Alisema pamoja na juhudi hizi wamekuwa wakikwamisha na benki mbalimbali ambazo zinachelewa kuwapatia mikopo jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma katika uzalishaji wao.
Msimamizi wa Kiwanda cha Singida Grains and Oil Mills, Jamal Juma akitoa taarifa kwa Kairuki alisema tozo mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kushindwa kutoa leseni ya athari za mazingira zimesababisha
kiwanda hicho kuchelewa kuanza kufanya kazi.
Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Ltd, Nelson Mwakabuta alisema ili kuongeza hamasa ya wanafunzi kuzingatia masomo hususan wa shule za msingi na kwa nia ya kukuza mahusiano mema mema na jamii, kampuni ina utaratibu wa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi tangu mwaka 2015.
Alisema mpaka sasa wanatoa huduma hiyo kwa shule za msingi 45 Arusha zenye jumla ya wanafunzi 65,743 na shule moja Singida yenye wanafunzi 1,288 na kuwa katika baadhi ya maeneo ya wakulima wametoa mbegu bora ya alizeti ili wakulima wavune
zaidi kwa ekari na kupata mafuta mengi kutoka kilo moja ya mavuno.

No comments:
Post a Comment