Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akitoa hotuba yake
wakati wa uzinduzi wa huduma ya CRDB Malkia ya Benki ya CRDB inayolenga
kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini. (Picha na Francis Dande).
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson, akitoa hoyuba yake wakati wa uzinduzi wa huduma ya CRDB Malkia ya Benki ya CRDB inayolenga kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini. Katika uzinduzi huo Benki ya CRDB imetangaza kupunguza riba ya mikopo kwa wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14, iliyofanyika leo katika hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akimpongeza Naibu Spika,
Dk. Tulia Ackson baada ya kutoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa
huduma ya "CRDB Malkia" ya Benki ya CRDB inayolenga
kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini.
Meneja wa Kitengo Huduma za Wanawake Benki ya CRDB, Rehema Shambwe, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
huduma ya "CRDB Malkia" ya Benki ya CRDB inayolenga
kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini.
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson (katikati), akifuatilia hotuba ya Meneja wa Kitengo cha Huduma za Wanawake Benki ya CRDB, Rehema Shambwe.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akizungumza
katika uzinduzi wa huduma ya CRDB Malkia ya Benki ya CRDB inayolenga
kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini. Katika uzinduzi huo
Benki ya CRDB imetangaza kupunguza riba ya mikopo kwa wajasiriamali
kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson (wa tatu kutoka kushoto),
akiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa huduma ya “CRDB Malkia”.
Na Irene Mark
BENKI ya CRDB imetangaza kupunguza riba kwa mikopo ya wanawake wajasiriamali inayopatikana kupitia huduma ya “CRDB Malkia” hadi kufikia asilimia 14 kwa mwaka.
Awali riba ya mikopo kwenye huduma ya CRDB Malkia ilikuwa asilimia 24 kwa mwaka.
Akihutubia baadhi ya watumiaji wa akaunti hiyo katika hafla ya uzinduzi wa “CRDB Malkia” iliyokuwa na kauli mbiu ya “Fanikisha Zaidi na CRDB Malkia”, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 Dk. Tulia Akson alisema hatua ya Benki ya CRDB kupunguza hiyo itasaidia wanawake wengi zaidi kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo.
“Kupungua kwa riba ina maana inapunguza mzigo mkubwa wa marejesho kwa wanawake na kuwafanya kuwa na fedha nyingi kwa ajili ya uwekezaji katika biashara zao na hivyo kunufaika zaidi,” alisema Dk. Tulia.
Alisema pamoja na tafiti kuonyesha wanawake wamekuwa na ushiriki mkubwa katika shughuli za kiuchumi nchini, kwa asilimia 54 ni asilimia 60 tu ya wanawake ndio wenye kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.
"Niwapongeze pia kwa kuboresha masharti ya dhamana ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kuweza mikopo,” aliongezea Dk. Tulia huku akiwataka wanawake pia wajitokeze kwa wingi kufungua akaunti ya Malkia itakayosaidia kufanikisha malengo yao kwa kujiwekea akiba kidogokidogo na kujenga imani kwa taasisi za fedha.
“Mimi ni mmoja wa wanawake waliofungua akaunti ya Malkia wakati ikianzishwa mwaka 2009, nimefurahi kuona leo hii Benki yetu ya CRDB ikifanya maboresho yenye lengo la kumkomboa mwanamke.
“...Nimefurahi kuona leo hii tukiwa tunajivunia kuwa nchi ya uchumi wa kati, Benki yetu ya CRDB inaendelea kutubeba wanawake na kuwezesha kufikia malengo yetu ya nchi na dunia katika kuwa na usawa katika ushiriki katika shughuli za maendeleo kama ilivyoainishwa katika mpango wa Maendeleo Endelevu 2030 wa umoja wa mataifa,” alisema Dk. Tulia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema huduma ya CRDB Malkia imelenga katika kumtambua, kumpa nafasi na kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kufikia malengo yake kupitia mikopo ya biashara na ujasiriamali, kujiwekea akiba kwa akaunti ya Malkia na mafunzo ya uendeshaji biashara.
“Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, Benki yetu tayari ilikuwa imekwisha toa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 600 kwa wanawake zaidi ya elfu 55,” alisema Nsekela huku akibainisha kuwa zaidi ya wanawake 30,000 tayari wameshajiunga na akaunti ya Malkia.
Nsekela alisema pamoja na mafanikio ambayo Benki ya CRDB imeyapata katika kumuwezesha mwanamke, bado idadi ndogo ya wanawake wamekuwa wakijitokeza kupata huduma kutokana na changamoto ya riba, masharti magumu ya dhamana na kukosa uelewa wa huduma za kifedha.
"Tukiwa Benki ya kizalendo inayothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu, tukasema ni vyema tukatafuta suluhisho la changamoto hizi ili kuweza kumsaidia mwanamke kufankisha malengo yake zaidi.
Nsekela alisema wanawake sasa hivi wataweza kupata mikopo kwa riba ndogo ya asilimia 14 kulinganisha na asilimia 24 iliyokuwa ikitozwa mwanzo huku masharti ya upatikanaji wa mikopo yakirahisishwa kwa kiasi kikubwa.
"Kupungua kwa riba kuna maana wanawake sasa wanaweza kukopa zaidi na kwa gharama nafuu kulinganisha na mwanzo hivyo kusaidia kufanikisha malengo yao kwa uharaka zaidi,” alisema Nsekela.
No comments:
Post a Comment