HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 02, 2020

WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA WATANZANIA KUUJENGA UCHUMI WA VIWANDA ENDELEVU

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika la Viwango nchini TBS baada ya kutembelea banda la shirika hilo lililopo kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba. (Picha na Francis Dande).
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (wa pili kushoto), akimsikiliza Ofisa wa Bunge, Peter Magati, baada ya kutembele banda la Bunge lililopo kwenye maonyesho hayo.
Akionja wine. 
Akisalimiana na viongozi wa Benki ya NBC.



NA TATU MOHAMED

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewataka Watanzania kujipanga kuujenga uchumi wa viwanda endelevu ili kulinda nchi ilipofikia katika uchumi wa kati.

Hatua hiyo imefika baada ya Benki ya Dunia juzi kuitambua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati mwaka 2020.

Waziri Bashungwa aliyasema hayo jana wakati alipotembelea maonesho ya 44 ya kimataifa ya biashara (sabasaba), yaliyokatika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alimpongeza Rais Magufuli na watanzania kwa ujumla kufikia mafanikio hayo.

Alisema Tanzania ilipanga kufika uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini ti umefikiwa kabla ya muda kunatokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais John Magufuli katika utekelezaji wa weledi na viwango vya ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Alisema misingi ya maandalizi ya kufikia uchumi wa kati ilijikita kwa watanzania kwenye uchumi wa viwanda edndelevu.

“Maandalizi ya sabasaba ya mwaka huu hasa wakati wa Covid-19, kama tusingekuwa na uchumi wa viwanda endelevu tungepata tabu sana kwasababu baada ya Covid 19 kuwa janga la dunia kila nchi ilikuwa ikiangalia uhitaji wake wa vifaa vya kujikinga,”alisema.

Alisema Tanzania ilijenga msingi wa viwanda chini ya ilani ya CCM ambapo viwanda vilizalisha vifaa kinga kama vitakasa mikono na ziada kwenda nje ya nchi huku barakoa zikizalishwa hapa nchini.

Alisema jambo hilo lingetokea wakati ambapo hakuna msingi wa viwanda nchi ingehangaika kuvipata nje ya nchi kutokana na kufungwa kwa mipaka.

Bashungwa aliongeza kuwa nchi inapoingia kwenye nchi ya uchumi wa kati, aliwataka watanzania kufanya kazi na kununua bidhaa zinazozalishwa na makampuni ya ndani na bidhaa zake.

“Ili kusherehekea na kuwa na uchumi wa kati endelevu tunapaswa kuwa soko la kwanza kwa bidhaa zinazozalishwa ndani tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa,”alisema.

Alisema hali hiyo itasaidia kutofanya watanzania kuwa soko la bidhaa za nchi za wengine.

“Rai yangu kwa watanzania ni kupenda bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi yetu ili mafanikio haya ya kufikia uchumi wa kati yawe matunda kwa watanzania vijana na wakinamama wanaotafuta ajira,”alisema.

Alifafanua kuwa mtanzania akinunua bidhaa zinazozalishwa nchini inatengeneza fursa kwa wazalishaji wa viwanda vya kati kushamiri katika uwekezaji wao.

No comments:

Post a Comment

Pages