NA MWANDISHI WETU
KUNDI
la muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ ROSTAM limenunua mashine mbili
za Oxygen ‘Oxygen Concentrator’ na mashuka 68 ili kukabidhi kwenye
hospitali za Tanga na Morogoro.
ROSTAM inayoundwa
na wasanii Ibrahim Mussa ‘Roma’ na Bonivanture Kabongo walianzisha
kampeni ya kuchangisha mashabiki wao fedha ili kununua vifaa vya hivyo
kupitia wimbo wao waliouachia hivi karibuni ‘Kaka Tuchat’.
Akizungmza
kuhusiana na suala hilo Roma alisema wanawashukuru mashabiki wao na
wote walioupenda wimbo wa ‘Kaka Tuchat’ kwa kuungana nao kufanikisha
jambo hilo.
“Siku zote waza na tamani kuwa Jua na
Mwezi, ili ukishindwa uangukie kwenye nyota, tumefanikiwa kufanya malipo
kwenye Bohari ya Madawa (MSD) na kununua mashine za Oxygen mbili na
mashuka 68.
“Kuanzia Julai mosi tutaenda
kuyakabidhi kwenye hospitali ambazo tumependekeza moja iwe morogoro
alipozaliwa na anapotoka Stamina na nyingine iwe Tanga alipozaliwa
Roma,” alisema Roma.
No comments:
Post a Comment