Lucy Owenya mtoto wa Mbunge wa zamani wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati akiomba kura katika uchaguzi wa kura za maoni za kumpata atakayegombea Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini kupitia Chadema.
Wakili Sisty Massawe ni miongoni mwa waliojitokeza kuwania nafasi ya kugombea Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini akizungumza na wapiga kura.
Wagombea wa nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi vijijini kupitia Chama cha Demokrasia (Chadema) wakisubiria matokeo wakati wa uchaguzi uliofanyika katika eneo la Garden ,kutoka kulia ni Lucy Ndesamburo ,Sisty Massawe na Emanuel Nyaki.
Na Dixon Busagaga, Moshi
MTOTO wa Mbunge wa
zamani wa Jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo ,Lucy Ndesamburo ameshinda
katika kura za maoni za kuwania kuteuliwa na Chama cha Demokrasia na maendeleo
(Chadema) kugombea Ubunge katika Jimbo
la Moshi vijijini.
Hii ni mara ya pili
kwa Lucy Ndesamburo kushinda katika kura za maoni katika jimbo hilo ambapo
mwaka 2015 alimshinda mpinzani wake Anthony Komu kwa zaidi ya kura 300 .
Katika kura hizo za
maoni, Lucy ameibuka na ushindi wa kura 129 sawa na asilimia 94. 2
huku wapinzani wake Emanuel Nyaki akipata kura 04 sawa na asilimia 2.9 na
Sisty Massawe akipata kura 4 sawa na 2.9.
Akitangaza matokeo ya
kura hizo za maoni, msimamizi wa uchaguzi, Ephata Nanyaro, amesema wajumbe
waliopiga kura ni 137 na kwamba mchakato unaoendelea kwa sasa ni wa kamati kuu
ya chama
Akizungumza Lucy,
baada ya matokeo hayo, mbali ya kushukuru, amewataka wajumbe kushirikiana ili
kuhakikisha chama kinashinda katika ubunge na hata nafasi za udiwani
Naye Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Kilawila, amewataka wanachama wa chama
hicho kuwa wamoja na kushikamana ili kuweza kukipatia chama hicho ushindi.
Katika uchaguzi wa
kura za maoni uliofanyika mwaka 2015 Lucy aliyekuwa mwanamke pekee katika
kinyang’anyiro hicho kati ya wagombea tisa, aliibuka mshindi kwa kupata kura
266 dhidi ya 25 alizopata Antony Komu.
Hata hivyo, baada ya
kushinda, kamati kuu haikurudisha jina lake na badala yake ilirudisha jina la
Komu ambaye sasa amehamia NCCR- Mageuzi
No comments:
Post a Comment